Loading...

Kauli ya Salah baada ya kuhusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid


Ikiwa imepita siku moja tangu kutolewa kwa ripoti iliyodai kwamba klabu ya Real Madrid inamtaka Mohamed Salah baada ya kuthibitisha kwamba klabu ya Barcelona imekamilisha usajili wa Philippe Coutinho.

Raia huyo wa Misri amechukua muda wake na kujibu tetesi hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Tangu ajiunge na Liverpool, ameonyesha uhai mkubwa sana katika Ligi Kuu ya Uingereza kwa kufunga magoli 17 na kutoa 'assist' 5 katika mechi 22.

Hesabu hiyo inazidi magoli ya Ronaldo, Benzema na Bale ukiyajumlisha kwa pamoja.

Kiwango chake cha kuvutia kimewapagawisha vigogo hao wa La Liga na hata kutaka kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kumnasa kwa dau kubwa zaidi.

Salah alichapisha ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Tweeter: ‘Kumekuwa na tetesi nyingi za uongo hivi karibuni, zitabakia kuwa hivyo wala hakutakuwa na maoni yoyote juu ya taarifa hizo.”
Kauli ya Salah baada ya kuhusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid Kauli ya Salah baada ya kuhusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 1/12/2018 05:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.