Loading...

Chelsea ina nia ya kumsajili nyota huyu wa Arsenal mwezi huu


Meneja wa Chelsea, Conte anatazamia kuongeza nguvu kwenye kikosi chake mwezi huu na ameshataja majina kadhaa ya wachezaji anaowahitaji. Jina jingine ambalo limeongezeka kwenye orodha yake ni la Alexis Sanchez.

Wakati sakata la mkataba mpya kati ya Sanchez na klabu ya Arsenal likiendelea, Wenger amekiri kwamba bado hajapokea ofa kutoka klabu yoyote ile kwa ajili ya uhamisho wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29. 


Lakini ripoti zinadai kwamba, Arsene Wenger atamwachia nyota huyo endapo atapata mtu anayefaa kuichukua nafasi yake mwezi huu. Inaaminika kwamba, washika bunduki hao wako tayari kukaa mezani kusikiliza ofa inayozidi pauni milioni 25.

Sanchez alikaribia kujiunga na Man City kwenye majira ya joto lakini dili hilo halikufanikiwa. Pep Guardiola pia amekiri kwamba, uwezekano wa kukamilisha uhamisho wa nyota huyo wezi huu ni mdogo sana. Klabu ya Manchester City sasa imepata upinzani kutoka kwa Conte. Kama ataweza kumsajili kiungo huyo, itakuwa ni pigo kubwa kwa City.


Akizungumza kuelekea mechi yao dhidi ya Arsenal, Conte alisema, “Sihusiki kwenye soko la usajili, ninatoa wazo lakini klabu ndio inaamua ni mchezaji gani inataka kumsajili, kuwekeza fedha zao.” Muitaliano huyo amemfanya Sanchez kuwa chaguo lake la kwanza kwenye orodha ya wachezaji anaowahitaji.

Kama Sanchez atajiunga na Chelsea, utakuwa ni uhamisho ambao utaongeza nguvu kubwa kwenye kikosi cha klabu hiyo. 

Conte amekiri kwamba hana kikosi chenye nguvu na kumpata mchezaji wa aina yake itakuwa msaada kwa meneja huyo raia wa Italia kuwa na nafasi kubwa ya kufanya uchaguzi.

Hata hivyo, kitakua kitendo cha kuvutia kuona kama Wenger atakuwa tayari kumuuza nyota huyo kwa hasimu wake.
Chelsea ina nia ya kumsajili nyota huyu wa Arsenal mwezi huu Chelsea ina nia ya kumsajili nyota huyu wa Arsenal mwezi huu Reviewed by Zero Degree on 1/03/2018 09:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.