Loading...

Mkutano wa kumi wa Bunge kuanza kesho mjini Dodoma


Mkutano wa kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaanza jesho mkoani Dodoma, huku mambo makuu manne yakitarajiwa kufanyika katika mkutano huo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kitengo cha habari, elimu kwa umma na mawasiliano inasema kuwa, shughuli ya kwanza kufanyika Bungeni hapo ni kiapo kwa wabunge wapya watatu.

Pia kuanzia mwanzo wa mkutano huo hadi kufika tamati yake, wastani wa maswali 125 ya kawaida yataulizwa na kutakuwa na maswali mengine papo hapo wastani wa 16 kwa waziri mkuu.

Jambo jingine ambalo linatarajiwa kujiri bungeni ni miswada miwili ya sheria kujadiliwa kwa hatua zote. Miswada hiyo ni ule wa marekebisho ya sheria mbalimbali na wa sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma, yote ni ya mwaka 2017.

Jambo jingine ni kamati 16 za kudumu za bunge kuwasilisha taarifa zao bungeni jambo ambalo baadhi ya wabunge wamesema wanalisubiri kwa hamu.

Kwa mujibu wa taarifa ya ITV, Mbunge wa viti maalum, Pendo Peneza anatarajia hoja yake inayohusiana na serikali kutoa bure taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari litajadiliwa.
Mkutano wa kumi wa Bunge kuanza kesho mjini Dodoma Mkutano wa kumi wa Bunge kuanza kesho mjini Dodoma Reviewed by Zero Degree on 1/29/2018 08:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.