Loading...

Mourinho: Mkhitaryan ataifaa sana Arsenal kuliko Manchester United


Kwa mujibu wa taarifa ya 'The Mirror', Jose Mourinho anaamini kuwa Henrikh Mkhitaryan atafaa sana akiwa Arsenal kuliko alivyokuwa Manchester United.

Meneja huyo wa United alisema kwamba, raia huyo wa Armenian atafurahia sana mchezo wa Arsene Wenger.

Mkhitaryan alitofautiana na Mourinho msimu huu, ambaye aliamua kumtoa kwa Arsenal kama sehemu ya makubaliano ya kumnasa Alexis Sanchez.

Wachezaji hao wawili walikamilisha taratibu zao za uhamisho wiki hii, na kwenye mazungumzo na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, Mourinho alitafakari juu ya kupoteza mchezaji mwenye "uwezo wa ajabu".

"Nafikiri ulikuwa ni uhamisho mzuri na uhamisho ni mzuri kama una faida kwa pande zote mbili," alisema meneja wa Manchester United.

"United na Arsenal zilifanya biashara nzuri, nilipoteza mchezaji mzuri, Bw Wenger naye alipoteza mchezaji mzuri, Alexis alihama kutoka klabu nzuri kwenda katika klabu yenye nguvu na Mkhitaryan alifuata klabu nzuri, hivyo ilikuwa ni biashara nzuri kwa kila mtu.

"Naamini Mkhitaryan ataenda kuwa mchezaji mzuri zaidi ya alivyokuwa United.

"Kwa mwaka mmoja na nusu nchini Uingereza, alishazoea hali ya mazingira na anaujua mchezo wa Arsenal. Nafikiri ulikuwa uhamisho mzuri wenye faida kwa kila mtu, ndio maana ninafuraha pia kwa Mkhitaryan kukamilsha hilo.

"Angeweza kufanya vizuri akiwa nasi, ningeweza kujifunza mengi kupitia ujuzi wake, labda, angechukuwa muda mrefu kuweza kuuzoea mchezo wetu, lakini sijutii lolote, kwa sasa yeye ni historia kwetu sisi, hivyo hisia ni nzuri kwa kila mtu na uhamisho maalum kwa timu pinzani ndani ya taifa kubwa, kitu ambacho naweza kusema inatakiwa kifanyike mara kwa mara."
Mourinho: Mkhitaryan ataifaa sana Arsenal kuliko Manchester United Mourinho: Mkhitaryan ataifaa sana Arsenal kuliko Manchester United Reviewed by Zero Degree on 1/27/2018 11:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.