Donald Trump akutana na Rais Paul Kagame
Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi baada ya Mkutano wa Viongozi na Watu Mashuhuri Kuhusu Uchumi na Biashara Duniani.
Mkutano huo wa Kagame na Trump umekuja wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kutoa kauli iliyotafsiliwa kama ni kuyakashifu mataifa ya Afrika.
Mkutano huo wa Kagame na Trump umekuja wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kutoa kauli iliyotafsiliwa kama ni kuyakashifu mataifa ya Afrika.
Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana ambapo amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyakashifu mataifa ya Afrika huku akikiri kutumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.
Wakati wa mkutano wake na Kagame, Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika huku akisifia kuwa mkutano wao huo ulikuwa “wa kufana sana”, na kueleza nchi hizo mbili kama washirika wa kibiashara ambao wanajivunia “uhusiano mzuri sana.”
Trump akifanya mazungumzo na Kagame |
“Ningependa kukupongeza, Bw Rais, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa … najua unaenda kuhudhuria mkutano wa kwanza karibuni. Tafadhali, fikisha salamu zangu.”
Kutoka kusoto ni mama Jeannette Nyiramongi Kagame, Rais Kagame, Rais Trump na Melania Trump
|
Donald Trump akutana na Rais Paul Kagame
Reviewed by Zero Degree
on
1/27/2018 12:21:00 PM
Rating: