Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 27 Januari, 2018


Real Madrid inaandaa pauni milioni 500 kwa ajili ya uhamisho wa nyota kadhaa toka Ligi Kuu ya Uingereza, huku kukiwa na majina kama Harry Kane, Eden Hazard na David de Gea kwenye orodha yao.

Celtic inakaribia kukamilisha dili la uhamisho wa chipukizi wa klabu ya Chelsea, Charly Musonda kwa mkopo.

Tottenham ina wakati mgumu kumbakisha Mauricio Pochettino baada ya Real Madrid kujitokeza kutaka huduma ya mkufunzi huyo.

Meneja wa West Brom, Alan Pardew anasema Salomon Rondon hatauzwa mwezi huu licha ya kwamba Chelsea imeonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Daily Mail)

Lucas Moura
Tottenham imefikia makubaliano na winga wa klabu ya PSG, Lucas Moura kuelekea uhamisho wa Mbrazil huyo kwa pauni milioni 25.

Arsenal watalazimika kuongeza ofa yao hadi pauni milioni 25 kama wanaitaka saini ya beki wa West Brom, Jonny Evans mwezi huu.

West Ham wana nia ya kumsajili Troy Deeney kama dili lao la uhamisho wa Daniel Sturridge litagonga mwamba, ingawa wanaweza kukutana na ushindani mkubwa kutoka Stoke City na Brighton kwenye mbio hizo za kuwania saini ya straika wa Watford.

Juventus inataka kumsajili Matteo Darmian kwa mkopo, huku wakiwa na lengo la kumnunua moja kwa moja kwenye majira ya joto, na Jose Mourinho yuko tayari kumruhusu Muitaliano huyo aondoke. (Sun)

Arsenal na Everton zinashindania saini ya Marcelo Brozovic kuotopa Inter Milan.

Arsenal imepata pigo kubwa kwenye dili la uhamisho wa mshambuliaji wa Genoa, Pietro Pellegri baada ya nyota huyo kuchagua kujiunga na klabu ya Monaco.

Faouzi Ghoulam
Manchester United iko tayari kulipa dau la pauni milioni 52.6 kwa aiji ya uhamisho wa beki wa klabu ya Napoli, Faouzi Ghoulam.

Jurgen Klopp amekataa kumwahidi Daniel Sturridge muda wa kutosha uwanjani kama atachagua kubaki Liverpool.

Meneja wa PSG, Unai Emery anasema kuwa Neymar atakuwa mchezaji bora wa dunia na kwamba atafanya hivyo akiwa na klabu hiyo ya Ufaransa.

Aliyekuwa wa Manchester United, Rene Meulensteen amemtaja Jesse Lingard kama "Andres Iniesta wa Uingereza". (Mirror)

Meneja wa klabu ya Borussia Dortmund, Peter Stoger amekiri kwamba klabu yake ina mpango wa kumuuza Pierre-Emerick Aubameyang.

Cristiano Ronaldo ameelezwa kuwa atauzwa na klabu ya Real Madrid kwenye majira ya joto - na kuna uwezekano mkubwa akajiunga na klabu ya Manchester United. (Star)

Alan Pardew
Meneja wa klabu ya West Brom, 
Alan Pardew anajikuta kwenye wakati mgumu kumbakisha Jonny Evans kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa mwezi Januari, huku kukiwa na klabu kama Arsenal na Manchester City, ambazo zinasubiria saini ya beki huyo.

Pep Guardiola anasema kuwa ratiba ngumu ya klabu ya Manchester City haitamfanya alitoe sadaka Kombe la FA. (Telegraph)

Antonio Conte ameeleza kuwa ni vigumu sana kuitumikia klabu ya Chelsea kama meneja wa muda mrefu. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 27 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 27 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/27/2018 12:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.