Loading...

TFF yaijibu Azam FC kuhusu ombi la kubadilishiwa mwamuzi


Azam FC inaamini mwamuzi Israel Nkongo atakayewachezesha dhidi ya Yanga leo, huwa hawatendi haki na wangependa aondolewe au kubadilishwa.

Lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeigomea Azam FC kuhusiana na ombi lake la kutaka mwamuzi wa mechi yake ya leo na Yanga, Israel Nkongo abadilishwe.

Juzi Alhamisi, Azam ilidaiwa kutinga TFF kuomba kubadilishiwa mwamuzi wa mechi hiyo kutokana na kutokuwa na imani naye.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema wao wanamwamini Nkongo na ndiyo maana wameamua kumpatia mechi hiyo kwa hiyo hawawezi kumbadilisha.

“Nkongo ni mwamuzi tunayemwamini na ana Beji ya Fifa na ndiye tuliona anafaa kuchezesha mechi hiyo, kwa hiyo hakuna kitakachobadilika,” alisema Kidau.

Mwaka 2012, Nkongo aliwahi kupigwa na baadhi ya wachezaji wa Yanga wakimtuhumu alikuwa akiibeba Azam katika mchezo wa ligi kuu kwenye Uwanja wa Taifa ambao Azam ilishinda mabao 3-1.
TFF yaijibu Azam FC kuhusu ombi la kubadilishiwa mwamuzi TFF yaijibu Azam FC kuhusu ombi la kubadilishiwa mwamuzi Reviewed by Zero Degree on 1/27/2018 12:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.