Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 6 Juni, 2024
Atletico Madrid wanataka kumsajili Julian Alvarez wa Manchester City, Manchester United wamejiunga na Liverpool katika harakati za kumnasa Leny Yoro na Galatasaray wanamtaka Anthony Martial.
Atletico Madrid wamewasiliana na wachezaji watatu wa Argentina Angel Correa, Rodrigo de Paul na Nahuel Molina ili kuuliza kuhusu upatikanaji wa mshambulizi mwenzao, mshambulizi wa Manchester City , Julian Alvarez, 24. (Marca)
Kkabu ya Paris St-Germain pia wanavutiwa na Alvarez. (Fabrizio Romano)
Manchester United wamejiunga na Liverpool katika harakati za kumsaka beki wa kati wa Ufaransa Leny Yoro mwenye umri wa miaka 18 kutoka Lille. (Marca)
Ombi la Manchester United haliwezekani na Real Madrid wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili Yoro. (Mail)
Klabu ya Besiktas ya Uturuki ilikuwa kwenye mazungumzo na meneja wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kabla ya kumteua meneja wa zamani wa Rangers Giovanni van Bronckhorst.
Galatasaray wana nia ya kumsajili fowadi wa Ufaransa Anthony Martial lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atalazimika kupunguza mahitaji yake ya mshahara baada ya kuondoka Manchester United. (ESPN)
Manchester City wanajiandaa kufanya mazungumzo na meneja Pep Guardiola, 53, kuhusu mustakabali wake. (Telegraph)
Tottenham wanatazamiwa kushindana na Aston Villa katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Conor Gallagher, 24, ambaye pia anasakwa na Atletico Madrid kwa pauni milioni 50. (Mail)
Barcelona wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Real Sociedad Mhispania Mikel Merino, 27. (Sport)
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Fulham kutoka Brazil, Andreas Pereira, 28, anasema atajadili mustakabali wake na wakala wake baada ya michuano ya Copa America msimu huu wa joto. (UOL)
Klabu ya Tottenham wanataka kumsajili Pereira, mwenye umri wa miaka 28. (Teamtalk)
West Ham wametoa ofa ya pauni milioni 6.8 kumnunua mlinzi wa Brazil Vitao mwenye umri wa miaka 24 kutoka Internacional. (Revista Colorada)
Newcastle wako kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumsajili beki wa Uingereza Lloyd Kelly, 25, ambaye Bournemouth wanasema ataondoka mwishoni mwa kandarasi yake msimu huu wa joto. Roma na Atletico Madrid pia wanavutiwa naye. (Sky Sports)
Klabu ya Bayern Munich wanataka kuongeza mkataba wa beki wa pembeni wa Canada Alphonso Davies, 23, na hawamtaki tena beki wa kushoto wa Arsenal na Ukraine Oleksandr Zinchenko, 27. (Sky Germany)
Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea na Brighton Graham Potter anatarajiwa kuchukua nafasi ya Arne Slot kama meneja mkuu wa Feyenoord. (1908)
Liverpool wanalenga kumsajili mlinda lango mpya huku wakijiandaa kumruhusu Caoimhin Kelleher 25 wa Jamhuri ya Ireland kuondoka Anfield msimu huu wa joto. (Football Insider)
Tottenham, Liverpool , Newcastle na West Ham wanavutiwa na mlinzi wa klabu ya Feyenoord Mholanzi Lutsharel Geertruida mwenye umri wa miaka 23. (AD)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 6 Juni, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
6/06/2024 09:44:00 AM
Rating: