Loading...

Kauli ya Drinkwater baada ya kusaini mkataba wa miaka 5 Chelsea


Danny Drinkwater rasmi awa mchezaji wa Chelsea baada ya kukamilisha taratibu za uhamisho kutokea Leicester City na kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu yake mpya.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Chelsea katika dirisha la usajili lililofungwa tarehe 31 mwezi Agosti kufuatia kusajiliwa kwa Willy Caballero, Antonio Rudiger, Tiemoue Bakayoko, Alvaro Morata na pia Davide Zappacosta.

Drinkwater alisema: Najisikia furaha sana kuwa mchezaji wa Chelsea na nina hamu ya kuanza kuitumikia klabu yangu mpya. Imekuwa ni safari ndefu kufika hapa lakini ninafuraha na ninatazamia kuisaidia klabu kushinda mataji mengine zaidi.

Mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea, Michael Emenalo aliongeza:Danny sio tu mshindi wa Ligi Kuu ya Uingereza lakini pia ana uzoefu na Ligi ya Mabingwa kitu ambacho ni faida kubwa sana kwetu sisi msimu huu. Ni mchezaji wa aina yake katika kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kutoa pasi za uhakika na kuwasili kwake kutasaidia kuimarisha safu yetu ya kiungo.’
Kauli ya Drinkwater baada ya kusaini mkataba wa miaka 5 Chelsea Kauli ya Drinkwater baada ya kusaini mkataba wa miaka 5 Chelsea Reviewed by Zero Degree on 9/02/2017 06:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.