Loading...

Yanga yapokea zaidi ya milioni 500 kutoka SportPesa


Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamepokea hundi ya mfano ya Sh. milioni 537.5 kutoka Kampuni ya Burudani na Michezo ya Kubashiri SportPesa baada ya kufanya vizuri katika msimu uliomalizika wa 2023/24.

Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni siku chake zimepita baada ya msimu wa mashindano kumalizika hapa nchini.

Akizungumza jijini jana, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha SportPesa, Sabrina Msuya, aliwapongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la FA na kucheza hatua ya robo fainali ya mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msuya alisema hayo ni mafanikio mazuri na hiyo imetokana na juhudi mbalimbali walizofanya katika msimu huu na hatimaye kushinda mataji hayo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas, naye aliwapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara tatu mfululizo.

“SportPesa siku zote imekuwa ikijivunia mahusiano ya kiudhamini kati ya kampuni na Young Africans na hapajawahi kutokea muda tukajutia kwa sababu tumejihusisha na klabu ambayo inaendeshwa kiweledi. Kwanza kabisa tungependa kupongeza uongozi ulioko chini ya Rais, Hersi Said, uongozi ambao umejenga timu ambayo ni imara, aina ya wachezaji ambao inawasajili, benchi la ufundi kiasi Yanga imekuwa ni timu inayojitosheleza kwa ushindani wa aina yake katika bara la Afrika.

Ni jambo ambalo SportPesa tunaona tumefikia malengo yetu. Kila tunachokiahidi kimkataba tumekitekeleza bila kuchelewa na Yanga inahitaji mdhamini wa sampuli kama SportPesa. Leo tumekabidhi mfano wa hundi ya Sh. milioni 537.5,” alisema Tarimba.

Aliwaomba Yanga kutobweteka na mafanikio hayo na badala yake kuboresha timu yao kwa sababu anaamini msimu wa mwaka 2024/25 utakuwa na ushindani zaidi.

Kwa upande wake, Hersi aliwashukuru wadhamini hao kwa namna ambavyo wameshirikiana na Yanga kama mdhamini mkuu katika kutekeleza mipango na majukumu ya kila siku.

“Nichukue nafasi hii kuishukuru SportPesa kwa kutekeleza kwa wakati makubaliano yaliyopo kwenye mkataba kwa kutoa bonus ya Sh. milioni 537.5 baada ya klabu yetu kutwaa ubingwa huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la FA.

Sisi kama Young Africans tumefurahi sana kupokea rasmi zawadi hii ya bonasi ambayo kimkataba kwa sisi kushinda Ligi Kuu, Kombe la FA na kufika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Ligi ya Mabigwa Afrika.

Huu ni msimu wa tatu mfululizo tumekuwa tukichukua ubingwa na kupata bonus hizi kutoka SportPesa. Tulianza na kuingia robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya hapo tumechukua taji la Ligi Kuu na mwisho tumechukua Kombe la FA, na leo (jana), hii tunawakabidhi makombe yote kama wadhamini wakuu”.

Rais huyo aliahidi Yanga itaendelea kujiimarisha ili kufanya vizuri zaidi katika msimu mpya wa mashindano.

"Tunawaahidi tutaendela kujenga timu imara ya ushindani ndani na nje ya Tanzania ili kuitangaza zaidi SportPesa ambaye ndiye mdhamini wetu mkuu,” alisema Hersi.

Aliongeza wamewapa mapumziko wachezaji wao na wanatarajia kuanza kambi rasmi kwa ajili ya msimu mpya mapema mwezi ujao.

SportPesa imetimiza miaka saba tangu kuanzishwa kwake pamoja na kuidhamini Yanga
Yanga yapokea zaidi ya milioni 500 kutoka SportPesa Yanga yapokea zaidi ya milioni 500 kutoka SportPesa Reviewed by Zero Degree on 6/06/2024 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.