Loading...

VIDEO: Ronaldo alivyoipoteza Bayern Munich kwenye uwanja wao wa nyumbani

Cristiano Ronaldo amemaliza ukame wa miezi saba kwenye ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuandika magoli mawili katika mchezo ambao Bayern Munich wamepoteza kwa magoli 2-1 dhidi ya Real Madrid.

Kwa sasa anafikisha magoli 100 na kuendelea kuwa kinara wa ufungaji Ulaya.

Arturo Vidal alipachika goli la kwanza lakini akakosa nafasi ya kuandika goli la pili baada ya kupaisha mkwaju wa penalti alioupiga.

Javi Martinez alilimwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu.

Bayern walitawaliwa baada ya kadi nyekundu na kujikuta muda mwingi wakiwa wanatafuta mpira.

Mlinda mlango Manuel Neuer, aliokoa mikwaju ya hatari ikiwemo ya Gareth Bale, Karim Benzema na Ronaldo.


VIDEO: Ronaldo alivyoipoteza Bayern Munich kwenye uwanja wao wa nyumbani VIDEO: Ronaldo alivyoipoteza Bayern Munich kwenye uwanja wao wa nyumbani Reviewed by Zero Degree on 4/13/2017 01:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.