Waziri Sospeter Muhongo atoa onyo kwa wanasheria 'wanaoifelisha' Tanesco
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kukosekana kwa uzalendo na uaminifu miongoni mwa wanasheria wa wizara hiyo kumesababisha wizara ya Nishati na Madini kuingia katika mikataba mibovu inayopelekea hasara kwa Taifa huku akipiga marufuku kwa taasisi zilizo chini ya wizara yake kuingia mikataba kabla ya kutoa taarifa kwa Wizara.
Waziri Muhongo ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo mjini Dodoma huku akisema kufuatia hatua hiyo watendaji wa wizara hiyo wamekuwa wakiingia katika mtego wa kusaini mikataba yenye kuinyonya nchi huku wanasheria wakiwa wanafahamu kinachoendelea
“Kitengo kinachotupatia maisha magumu katika Wizara hii ni kitengo cha sheria, kwahiyo kitengo cha sheria Katibu mkuu,Naibu waziri na Waziri wasipokuwa makini kusoma documents zinazotoka huko basi ni hatari kabisa yaani wote waliopo ni vijana wengine wana masters wana nini eeh inakuwaje kweli unampatia kiongozi wako documents ina makosa na ukiangalia makosa mengine na hata kama wengine hatukusoma sheria unashangaa unasema huyu ni mwanasheria gani anaandika hivi? , alisisitiza na kuhoji.
Aidha Waziri Muhongo akatoa mfano jinsi wanasheria wanavyofumbia macho Mikataba mibovu.
“Kwa mfano ntawapatia mfano wa Kigagati Mrongo wanasheria wanaandika wanasema iwapo Tanesco hawatanunua huo umeme ni lazima Tanesco ipigwe penati full stop halafu wanataka Waziri usaini yaani huyo ni Mtanzania gani hajiulizi je, Tanesco wasipopewa umeme na anayezalisha umeme asipigwe penati? alihoji.

Reviewed by Zero Degree
on
4/13/2017 01:45:00 PM
Rating: