Mwigulu Nchemba apiga marufuku suala la wabunge kuhojiwa nje ya Dodoma
Badala yake, ameagiza kuwa chombo chochote kinachotaka kufanya hivyo kifanyie hapo hapo bungeni.
“Chombo chochote kinachotaka kufanya mahojiano na wabunge waje wafanyie hapa bungeni, waje wachukue maelezo yao hapa kwa waheshimiwa wabunge,” aliagiza Mwigulu wakati akitoa ufafanuzi wa hoja za wabunge zilizoelekezwa katika wizara yake, wakati wakichangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyowasilishwa wiki iliyopita.
Alisema wabunge wapo bungeni hapo kwa ajili ya shughuli za kitaifa na kuwakilishwa wananchi wao, hivyo chombo chochote kinachotaka kufanya mahojiano na mbunge yeyote, kije kifanye nao bungeni.
Alisema kitendo cha kumsafirisha mbunge kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam au hadi mahali pengine, ni hatari na gharama kubwa kusafirisha, vyombo hivyo vinaweza kufanyia mahojiano hapo hapo bungeni badala ya kumsafirisha mbunge.
Mwigulu alisema ofisa anayetaka kufanya mahojiano ndiye anatakiwa kufunga safari akiwa na maelezo ya kumhoji mbunge badala ya kumsafirisha.
Alisema uamuzi huo hauingilii masuala yanayohusu utaratibu wa kumkamata mbunge yaliyo ndani ya utaratibu wa Spika wa Bunge, anazungumzia yale ambayo yanahusu vyombo vilivyo chini yake ambavyo kama vinataka kumhoji mbunge vije na maelezo hapo hapo bungeni.
Baadhi ya wabunge ambao wamekwisha kukamatwa wakiwa Dodoma na kusafirishwa ni Tundu Lissu na Gobless Lema, wote wa Chadema.
Kuhusu uhalifu, alisema serikali haitaruhusu kuendelea kufanyika uhalifu, na hivyo wizara yake ina wajibu wa kuhakikisha haufanyiki kwa kufuata misingi ya haki na sheria.
Mwigulu alisema nchi hii inaongozwa kwa utawala wa sheria, hakuna mtu ambaye yupo juu yake, hivyo ni wajibu wa wizara yake kuhakikisha jambo inalotoa hadharani lazima liwe limefanyiwa uchunguzi.
Alisema wabunge wengi, walikuwa wakihoji kwanini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi hajatoa tamko kuhusu kukamatwa, kutishiwa silaha na kutekwa kwa watu, naye alisema anafanya kazi kwa kutegemea taarifa anazoletewa na vyombo vyake vya uchunguzi.
Mwigulu alisema anafanya kazi kwa mujibu wa sheria na hivyo kuchelewa kwake kusitafsiriwe kwamba anafanya makusudi, bali anategemea taarifa ya vyombo na akifanya kabla vyombo havijafanya kazi yake, vinaweza kuacha au kushindwa kufanya kazi vizuri.

Reviewed by Zero Degree
on
4/13/2017 02:16:00 PM
Rating: