Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 16 Februari, 2018

Neymar akisalimiana na Cristiano Ronaldo
Klabu ya PSG imesema kuwa hakuna nafasi kwa Neymar kuondoka Ufaransa kwenye majira ya joto, licha ya kuwepo kwa uvumi mkubwa unaomhusisha mshambuliaji huyo na uhamisho kwenda Real Madrid.

Michy Batshuayi amesema kuwa hafikirii kuhusu hatima ya maisha yake ya soka kwa sasa na badala yake anakazani kufanya vyema kila anapopata nafasi katika kikosi cha Borussia Dortmund. (ESPN)

Arsenal ina matumaini ya kufanikiwa kumrejesha Oguzhan Ozyakup kwenye majira ya joto.

Klabu ya Tottenham inatarajiwa kumpa Maurcio Pochettino ofa ya mkataba mpya wenye maslahi mazuri zaidi ya mkataba wake wa sasa.

Timu ya Taifa ya Uskoti imethibitisha kumteua Alex McLeish kuwa kama meneja mkuu. (talkSport)

Real Madrid inafanya mpango wa kutumia pauni milioni 120 kumnasa kiungo wa Manchester United, Paul Pogba kwenye majira ya joto.

Joe Hart yuko tayari kujaribu bahati yake nje ya Ligi Kuu ya Uingereza na kukubali uhamisho mwingine wa mkopo kwenye majira ya joto baada ya kuwa na wakati mgumu katika klabu ya West Ham.

Antonio Conte ameahidi kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha Chelsea kitakachocheza dhidi ya Hull City kwenye FA Cup, huku Alvaro Morata akitarajiwa kuanza. (Sun)

Jose Morais
Klabu ya Barnsley imemteua Jose Morais kama meneja mkuu na kumpa mkataba wa miezi 18.

Klabu ya Liverpool inafanya mpango wa kumsajili golikipa wa Roma, Alisson anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 62 kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili kwenye majira ya joto.

Aliyekuwa meneja msaidizi wa klabu ya Chelsea, Ray Wilkins amesema kuwa klabu hiyo inatakiwa kuhakikisaha Eden Hazard haondoki kwenda Real Madrid.

Jose Mourinho amekanusha taarifa zinazodai kuwa ametofautiana na kiuongo wa klabu hiyo, Paul Pogba.

Pep Guardiola amethibitisha kurejea kwa Gabriel Jesus kwenye mazoezi baada ya kuwa nje akiuguza majeraha yake, lakini anaweza akaikosa mechi ya FA Cup dhidi ya Wigan siku ya Jumatatu. (Sky Sports)

John Terry anafanya mpango wa kurejea Chelsea kama mmoja wa wakufunzi wa benchi la ufundi mwishoni mwa msimu huu, akiamini kuwa hiyo itamsadia kupata fursa ya kuino 'The Blues' miaka ijayo.

Mshambuliaji wa Brazil, Malcom ameziweka Arsenal na Tottenham katika mkao wa kula baada ya kueleza kuwa klabu ya Bordeaux inaweza kumruhusu aondoke kwenye majira ya joto. (Mirror)

Paul Pogba ameamua kufanya kazi kwa bidii pamoja na tofauti zozote zilizopo kati yake na Jose Mourinho kufuatia ripoti zilizodai kuwa nyota huyo anajutia kurejea Manchester United.

Mauricio Pellegrino anakiri kuwa mechi tano za Southampton zinazofuata ni muhimu sana kwa klabu hiyo kuhakikisha haishuki daraja kwenye Ligi Kuu ya Uingereza na kuendelea na michuano ya FA.

Sadio Mane
Sadio Mane anakiri kushuka kiwango katika msimu wake wa pili Liverpool, lakini anasema kuwa hakuacha kujiamini hata siku moja baada ya kurejea uwanjani kwa kufunga hat-trick ya kushangaza dhidi ya Porto. (Telegraph)

Chelsea inaweza kubadili mfumo kufuatia kuwasili kwa Olivier Giroud, Antonio Conte akifiria juu ya uwezekano wa kumwanzisha Mfaransa huyo pamoja na Alvaro Morata.

Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku amekiri kuwa ana nia ya kurejea katika klabu yake ya awali, Anderlecht kabla hajaamua kuachana na mchezo wa soka. (Express)

Inasemekana kuwa Gary Cahill anahisi ukiwa na kukata tamaa baada ya Ryan Mason kulazimishwa kustaafu mchezo wa soka baada ya kugongana vichwa na nahodha huyo wa Chelsea msimu uliopita.

Sergio Ramos anadai Zinedine Zidane anaweza asiwe mkufunzi wa Real Madrid msimu ujao kwa kusema kuwa meneja huyo anaweza akahitaji mapumziko kwa muda.

Baba mzazi wa Neymar amesema kuwa mwanaye ni kama amezungukwa na tai, baada ya kuibuka kwa mdahalo juu ya kiwango cha mshambuliaji huyo katika mechi ya PSG dhidi ya Real Madrid. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa klabu ya Watford, Richarlison amekataa kukanusha taarifa za uhamisho wake kwenda katika timu pinzani ndani ya Ligi Kuu, huku Arsenal, Chelsea na Tottenham zikiwa na nia ya kumnasa nyota huyo.

Alvaro Morata ameambiwa na Antonio Conte atumie nafasi ya kurejea kwake kwenye mchezo wa Chelsea dhidi ya Hull City kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona wiki ijayo. (Star)

Dejan Lovren anasema kuwa klabu ya Liverpool ina imani ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa baada ya kuibuka na ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Porto katika raundi ya 16 bora.

Erik Lamela
Klabu ya Tottenham inaweza kuongeza mkataba wa Erik Lamela hadi 2020, kitu ambacho kinaweza kuzikatisha tamaa klabu za Ligi ya Serie A zinazowania saini ya nyota huyo. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 16 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 16 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/16/2018 01:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.