Loading...

Mvua yasababisha vifo vya watu watano mkoani Dodoma


Mvua zilizonyesha siku za hivi karibuni zimesababisha vifo vya watu zaidi ya 5 katika sehemu tofauti tofauti mkoani Dodoma.

Akielezea tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, amesema vifo hivyo vimetokea kwa nyakati tofauti tofauti kwenye baadhi ya maeneo ya mkoa wa Dodoma, lakini vimesababishwa na maafa ya mvua hizo.

“Ni maeneo mbali mbali kwa mfano juzi ile kulikuwa na watu watano walikuwa wamesimama kwenye choo kikatitia, watatu wakapona wawili wakafariki, jana kuna mtu alikuwa anavuka mto na baiskeli akabebwa na maji na lakini pia eneo la Bahi kulikuwa na mtu ambaye amengia kwenye dimbwi, alichukuliwa na maji, na leo kwenye machimbo ya dhahabu yasiyo rasmi, walikuwa watatu, wawili wakaokoka mmoja amefariki, na mama mmoja alipigwa na radi kule Chamwino”, amesema Kamanda Muroto.

Kutokana na matukio hayo Kamanda Muroto amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha nchini, ili kuepuka madhara kama hayo na mengineyo.
Mvua yasababisha vifo vya watu watano mkoani Dodoma Mvua yasababisha vifo vya watu watano mkoani Dodoma Reviewed by Zero Degree on 1/05/2018 07:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.