Loading...

Mwamuzi amrushia teke mchezaji kisha amtoa nje kwa kadi nyekundu nchini Ufaransa

RefaTony Chapron alionekana kumrushia teke mchezaji wa Nantes, Diego Carlos
Mechi kati ya Paris St-Germain na klabu ya Nantes nchini Ufaransa ilikumbwa na utata baada ya mwamuzi kuonekana kumrushia teke mchezaji.

Mwamuzi huyo, Tony Chapron alifanya hivyo baada ya kugongana na mchezaji huyo wa klabu ya Nantes, Diego Carlos.

Diego Carlos akitolewa uwanjani na Tony Chapron
Baada ya hilo, alimpa mchezaji huyo kadi ya pili ya manjano na kumfukuza uwanjani kufuatia kisa hicho muda wa ziada wa mechi.

Nantes walimaliza mechi wakiwa wachezaji 10.

Mwenyekiti wa Nantes Waldemar Kita amesema Chapron anafaa kupigwa marufuku kwa miezi sita kwa sababu ya uamuzi huo wenye utata.

Ameongeza kuwa: "Sitaki kuamini kwamba alifanya hivyo makusudi."

PSG walipokuwa wanashambulia eneo la hatari la Nantes, Carlos alimgonga Chapron kwenye kisigino katika kile kinachoonekana kuwa ajali.

"Ni mzaha," Kita aliambia runinga moja ya Ufaransa.

"Nimepokea ujumbe kutoka pande mbalimbali duniani kuniambia kwamba huyu mwamuzi alifanya mzaha tu.

"Nikizungumzia hili sana, nitaitwa kujibu maswali na kamati ya maadili. Hatuna haki ya kusema chochote."

PSG walishinda mechi hiyo yao ya kwanza baada ya mapumziko ya msimu wa baridi, bao lao pekee likifungwa na Angel di Maria dakika ya 12 uwanjani Stade de la Beaujoire.

Ushindi huo, bila mchezaji wao ghali zaidi Neymar aliyenunuliwa £200m - uliwaweka alama 11 mbele kileleni Ligue 1.

Meneja wa Nantes Claudio Ranieri alisema: "Jambo mbaya zaidi litakalomtokea Diego Carlos ni kwamba atapigwa marufuku kucheza mechi moja. Ilikuwa mechi nzuri kwetu tukisahau bao ambalo lilikataliwa kwa sababu ya kuotea na pia yaliyomsibu Diego Carlos."
Mwamuzi amrushia teke mchezaji kisha amtoa nje kwa kadi nyekundu nchini Ufaransa Mwamuzi amrushia teke mchezaji kisha amtoa nje kwa kadi nyekundu nchini Ufaransa Reviewed by Zero Degree on 1/16/2018 07:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.