Loading...

"Nimekuja kuondoa kichefu chefu cha maendeleo" - Dkt. Mollel

Mgombea Ubunge wa jimbo la Siha (CCM), Dk. Godwin Mollel
Mgombea Ubunge wa jimbo la Siha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Godwin Mollel amefarijika kuona bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye mkutano wake wa Makiwalu wakati akifanya kampeni za kugombea Ubunge wa jimbo.

Mollel ambaye alikuwa Mbunge wa jimbo la Siha kupitia CHADEMA na baadaye kujiuzulu na kwenda CCM na sasa amerudi tena kwenye jimbo hilo hilo akigombea Ubunge kupitia CCM, katika mkutano wake wananchi walikwenda na kufunga bendera ya CHADEMA na yeye kukiri kuwa bado anawapenda watu ambao walipambana naye awali mpaka kupata Ubunge kupitia CHADEMA.

"Niwaambie makamanda bado nina wapenda na kuwaheshimu ndiyo maana nimefarijika kuona bendera hizi mbili (CHADEMA) na (CCM) zipo hapa lakini mmeniwekea kwa namna nzuri kwamba mmeiweka ile juu na mmeonyesha dalili kwamba tutaishusha hii ya chini tuendelee kujenga Siha, mimi leo ni limao nimekuja kuondoa kichefu chefu cha maendeleo na watu wapate maendeleo" alisema Mollel.

Mbali na hilo Dkt. Mollel amedai kuwa anakumbuka mchango wa makanda hao ambao waliweza kusimama na yeye na kulinda kura mpaka siku alipotangazwa kuwa Mbunge wa jimbo la Siha kupitia CHADEMA.
"Nimekuja kuondoa kichefu chefu cha maendeleo" - Dkt. Mollel "Nimekuja kuondoa kichefu chefu cha maendeleo" - Dkt. Mollel Reviewed by Zero Degree on 1/29/2018 02:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.