Loading...

Orodha ya mwisho ya Florentino Perez ya wagombea watatu wa nafasi ya 'Zizou'

Mkufunzi wa Real Madrid, Zinedine Zidane 'Zizou'
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane anaweza asiendelee kuinoa klabu hiyo kama hatafanikiwa kutwaa taji lolote mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti ya 'Don Balon', Mfaransa huyo anatambua kuwa yuko katika hatari ya kutimuliwa na kwamba anatakiwa atwae moja kati ya mataji matatu muhimu kama atataka kuendelea kukalia benchi ya Real Madrid msimu ujao.

Kwa upande wake, Florentino Pérez anadhani itakuwa ni vugumu sana kiasi kwamba amefikia hatua ya kuanza kusaka mkufunzi mwingine wa kumrithi 'Zizou'. Ambapo taarifa hiyo imeeleza kwamba rais huyo wa klabu ya Real Madrid ameibuka na orodha fupi yenye majina matatu ambayo yanatarajiwa kutwaa nafasi hiyo.

Kulingana na taarifa hiyo, chaguo la kwanza la Florentino Pérez, inabakia kuwa Joachim Löw. Inadaiwa Mjerumani huyo amemwigia sana moyoni raisi huyo wa Real Madrid, huku kukiwa na uvumi unaodai kwamba kocha huyo yuko tayari kuondoka Ujerumani baada ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Majina mengine yanatoka Ligi Kuu ya Uingereza. Jina la kwanza kabisa la pili kwenye orodha hiyo likiwa ni la Mauricio Pochettino. Inadiwa meneja huyo wa Tottenham anaipenda sana bodi ya klabu ya Real Madrid, huku jina la tatu likiwa la Jürgen Klopp, ingawa klabu hiyo inatambua kabisa itakuwa vigumu kumpata meneja huyo kutoka Liverpool.
Orodha ya mwisho ya Florentino Perez ya wagombea watatu wa nafasi ya 'Zizou' Orodha ya mwisho ya Florentino Perez ya wagombea watatu wa nafasi ya 'Zizou' Reviewed by Zero Degree on 1/23/2018 07:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.