Loading...

Mch. Peter Msigwa anashikiliwa na jeshi la Polisi


Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kutokana na matukio ya kiuharifu yanayotokea mjini Iringa.

Mbunge huyo anahojiwa kuhusu kuchomwa nyumba ya Katibu wa UVCCM na kuvunjwa Nyumba ya Diwani aliyehamia CCM akitokea CHADEMA.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Julius Mjengi amethibitisha kushikiliwa kwa Mchungaji Peter Msigwa ambapo ameeleza anahojiwa kuhusu matukio ya uvunjwaji wa nyumba ya aliyekuwa diwani wa kata ya Mwangata kupitia chadema aliyejiuzulu na kujiunga na CCM pamoja na tukio la kuchomwa moto kwa nyumba aliyokuwa akiishi katibu wa UVCCM Iringa mjini.
Mch. Peter Msigwa anashikiliwa na jeshi la Polisi Mch. Peter Msigwa anashikiliwa na jeshi la Polisi Reviewed by Zero Degree on 1/23/2018 06:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.