Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 18 Januari, 2018
Gareth Bale |
Juventus wameanza mazungumzo juu ya uhamisho wa beki wa klabu ya Arsenal, Hector Bellerin. (Express)
Meneja wa Arsenal, Arsene Wnger anasema kuwa uhamisho wa Alexis Sanchez kwenda Manchester United unakaribia kukamilika ndani ya masaa 24 yajayo, huku Henrikh Mkhitaryan akitarajiwa kutua Emirates.
Swansea ina nia ya kumrejesha mshambuliaji wa klabu ya West Ham, Andre Ayew. (Sky Sports)
Andy Carroll ameiambia West Ham kuwa hawezi kufanya mazoezi huku klabu ya Chelsea ikionyesha nia ya kutaka kumsajili - lakini vipimo vya majeraha katika kifundo cha mguu havijabaini tatatizo lolote kwa nyota huyo.
Jordy Clasie ana matumaini ya kuufanya uhamisho wake wa mkopo kwenda Club Brugge kuwa mkataba wa kudumu na kusema kwamba kipindi chote ambacho aliitumikia Southampton kilikuwa cha kutisha sana.
Kiungo wa klabu ya Newcastle, Henri Saivet anatarajiwa kuhamia Montpellier kwa dau la pauni milioni 5. (Mirror)
Andy Carroll |
West Ham wamejiandaa kumuuza mshambuliaji wao, Andy Carroll kwenda Chelsea lakini wanaweza kumtaka Michy Batshuayi kwa mkpo kama sehemu ya makubaliano yao.
Manchester United wameanza mazungumzo na David de Gea juu ya mkataba mpya kumshawishi aachane na Real Madrid.
Sevilla na Inter Milan zinavutiwa na uwezo wa mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge. (Telegraph)
Alexis Sanchez anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kulipwa pauni 500000 kwa wiki baada ya kukubali kujiunga na Manchester United kwa mkataba wa pauni milioni 118.3.
Wakala wa Pierre-Emerick Aubameyang na baba mzazi wa nyota huyo wa klabu ya Borussia Dortimund wamesafiri kwenda London kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 53 kwenda Arsenal.
West Ham inadai kwamba, wazo la Chelsea kumsajili Andy Carroll kwa mkopo ni matusi kwa mshambuliaji huyo anayelipwa pauni 100,000 kwa wiki.
Manchester City itatumia pauni milioni 23.5 kukamilisha usajili wa beki wa klabu ya West Brom, Jonny Evans.
Rafa Benitez atafikiria kuhusu future yake kama meneja wa Newcastle mwishoni mwa msimu huu.
Liverpool wanakataa kumruhusu Ben Woodburn ajiunge na aliyekuwa meneja wa Wales, Chris Coleman kwa mkopo katika klabu ya Sunderland.
Huddersfield inatarajiwa kumsajili kiungo wa Chievo na raia wa Ubelgiji, Samuel Bastien kwa pauni milioni 3.5. (Sun)
Watford inategemea kufanya mazungumzo zaidi na klabu ya Leicester juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa klabu hiyo, Islam Slimani wiki hii.
Watford inategemea kufanya mazungumzo zaidi na klabu ya Leicester juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa klabu hiyo, Islam Slimani wiki hii.
Inigo Martinez |
Manchester City waongeza juhudi katika kuwania saini ya beki wa klabu ya Real Sociedad, Inigo Martinez.
Mashabiki wa Newcastle wenye hasira kali wamemtaka Mike Ashley aiuze klabu hiyo kuiweka katika mazingira ya kufanikiwa zaidi.
Mshambuliaji wa Watford, Stefano Okaka anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kwenda Marseille. (Star)
Real Madrid inatarajia kuwasajili washambuliaji watatu akiwemo mshambuliji wa PSG na raia wa Brazil, Neymar, Eden Hazard wa Chelsea na Robert Lewandowski wa Bayern Munich. (Marca)
Liverpool wamekataa ofa ya uhamisho wa mkopo kumwachia Daniel Sturridge kwenda Sevilla kwa kipindi chote kilichobakia katika msimu huu.
Swansea wanamfuatilia mshambuliaji wa AC Milan, Andre Silva, ambaye anapigania kung'ara katika Serie A tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea FC Porto.
Tottenham wanatazamia kumpa mkataba mpya Christian Eriksen huku kukiwa na tetesi nyingi zinazomhusisha nyota huyo na Juventus.
Richarlison atafikiria kuhusu mstakabali wa maisha yake katika klabu ya Watford kwenye majira ya joto, lakini klabu yake haina nia ya kumuuza mwezi huu.
Jon Flanagan |
Mstakabali wa maisha ya Jon Flanagan katika klabu ya Liverpool uko shakani baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 siku ya Jumatano. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 18 Januari, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
1/18/2018 04:16:00 PM
Rating: