Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 25 Januari, 2018

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte
Antonio Conte amekiri kwamba Chelsea haina uwezo tena wa kushindana na vilabu vya Manchester kwa suala zima la matumizi ya pesa kwenye usajili.

Uhamisho wa Edin Dzeko kwenda Chelsea unakwamishwa na wakala wa nyota huyo, ambaye anataka kibali kabla ya kusafiri kwenda London.

Aston Villa inakaribia kukamilisha taratibu za uhamisho wa mkopo wa beki wa kati wa klabu ya Manchester United, Axel Tuanzebe.

Manchester United na Manchester City zitaingia kwenye ushindani mkubwa tena, safari hii ikiwa ni kujaribu kumnasa kiungo wa klabu ya Nice, Jean Michael Seri.

Leigh Griffiths hana nia ya kuondoka Celtic, licha ya kuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza. (Express)

Ray Parlour ameishauri klabu ya Arsenal ihakikishe inakamilisha dili la uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang.

Robert Pires amemtetea Alexis Sanchez kwa kusema kuwa pesa sio sababu iliyomfanya ajiunge na Manchester United bali ni hali ya Arsenal kutokuwa na tamaa ya mafanikio. (TalkSport)

Daniel Sturridge
Liverpool inasita kumruhusu Danny Ings aondoke, huku Daniel Sturridge akiwa katika hatihati ya kuondoka Anfield.

Alberto Moreno lazima arejeshwe kwenye mipango ya Liverpool haraka baada ya kurejea mazoezini akitokea majeruhi tangu mwezi Decemba.

Klabu ya Monaco imekubali kumuuza mshambuliaji wao Guido Carrillo, kwenda Southampton kwa pauni milioni 19.2.

Lokomotiv Moscow ya Urusi inavizia saini ya nyota wa klabu ya Liverpool, Lazar Markovic. (Telegraph)

Klabu ya Leganes imetoa Real madrid nje ya michuano ya Copa del Rey katika dimba la Santiago Bernabeu.

De Bruyne: Manchester City itaendelea kung'ara bila Alexis Sanchez.

Meneja wa klabu ya Barcelona, Ernesto Valverde anasema klabu hiyo haina mpango wa kusajili beki mwingine licha ya kuondoka kwa Javier Mascherano.

Arsenal imetinga fainali ya Kombe la Carabao baada ya kuitoa Chelsea kwa kichapo cha goli 2-1.

Aymeric Laporte
Manchester City iko tayari kulipa pauni milioni 57 kumnasa beki wa klabu ya Athletic Bilbao, Aymeric Laporte. (ESPN)

Borusia Dortmund imeikataa ofa ya zaidi ya pauni milioni 50 kutoka klabu ya Arsenal kwa ajili ya uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang.

Klabu ya Roma imekanusha kukubali dili la uhamisho wa Edin Dzeko kwenda Chelsea.

West Ham inakaribia kumnasa kiungo wa klabu ya Inter Milan na timu ya taifa ya Ureno, Joao Mario.

Klabu ya Rangers imekubali dili la uhamisho wa kiungo wa klabu ya Hamiliton Academical, Greg Docherty. (Sky Sports)

Meneja mpya wa Wales, Ryan Giggs amethibitisha kuzungumza na Paul Scholes kuhusu kujiunga na benchi lake la ufundi.

Gareth Southgate yuko tayari kumjumuisha Jack Wilshere kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia.

Arsenal inatazamia kumsajili beki wa klabu ya Mainz, Abdou Diallo. (Mirror)

Salomon Rondon
Liverpool na Everton zitashindania saini ya mshambuliaji wa klabu ya West Brom, Salomon Rondon mwezi huu.

Meneja msaidizi wa klabu ya Leicester, Michael Appleton amekanusha taarifa zinazodai anataka kurejea Oxford United.

Manchester City inaweza kuingia kwenye makubaliano na klabu ya Atletico Madrid kuhusu dili la kubadilishana mshambuliaji wao, Sergio Aguero, ili imchukue Antoine Griezmann.

Kiungo wa West Ham, Pedro Obiang anawindwa na klabu ya Inter Milan.

Aliyekuwa beki wa klabu ya Arsenal na Manchester City, Bacary Sagna anaweza kujiunga na Benevento ya Serie A. (Sun)

Kevin De Bruyne anasisitiza kwamba Manchester City haina shida na Alexis Sanchez.

Klabu ya Bordeaux inamtaka straika wa Middlesbrough, Martin Braithwaite kwa mkopo, huku kukiwa na wazo jingine la kumnunua kwa pauni milioni 7.

Aymeric Laporte ameiambia Athletic Bilbao kuwa anataka kujiunga na vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester City.

Baba Rahman
Beki wa kushoto wa klabu ya Chelsea, Baba Rahman anatarajiwa kurejea katika klabu ya Schalke kwa mkopo.

Golikipa wa timu ya taifa ya Sweeden chini ya miaka 21, Pontus Dahalberg anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na meneja mpya wa klabu ya Watford, Javi Gracia.

Stoke City iko miongoni mwa vilabu vinavyowania saini ya mshambuliaji wa Hertha Berlin, David Selke.

Newcastle United imeambia iboreshe ofa yao ya pauni milioni 14 kama inataka kumnasa mshambuliaji wa Feyenoord, Nicolai Jorgensen. (Daily Mail)

Ombi la klabu ya Chelsea kuwasajilli nyota wawili wa klabu ya Roma, Edin Dzeko na Emerson Palmieri limekubaliwa. (Guardian)

Mshambuliaji wa Leicester, Islam Slimani, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Stamford Bridge, alishuhudia mechi ya nusu fainali ya Carabao kati ya Arsenal na Chelsea. (Star)

Brendan Rodgers
Brendan Rodgers amezungumzia kuhusu kusajili mchezaji atakayechukua nafasi ya Moussa Dembele kama Mfaransa huyo atauzwa na klabu ya Celtic mwezi huu na pia anaweza kusajili wachezaji wengine zaidi. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 25 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 25 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/25/2018 12:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.