Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 5 Januari, 2018

Arturo Vidal
Chelsea wamempa Arturo Vidal ofa ya mkataba wa miaka minne wenye thamani ya pauni milioni 13.4 kwa kila msimu aondoke Bayern Munich.

Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata amekuwa akiwasiliana na Real Madrid kuwapa onyo kuhusu mipango ya Barcelona kumsajili Philippe Coutinho.

Barcelona wameikataa nafasi waliyopewa kumsajili beki wa Chelsea, David Luiz.

Meneja wa Brighton, Chris Hughton ameionya West Ham kwamba, Lewis Dunk hauzwi, lakini Jamie Murphy anajiunga na Rangers kwa pauni milioni 1. (Star)

Kiungo wa klabu ya Liverpool, Emre Can amefikia makubaliano na klabu ya Juventus kuhusiana na uhamisho wake kwenda Italia kwenye majira ya joto.

Cenk Tosun
Cenk Tosun atafanyiwa vipimo vya afya leo Ijumaa kukamilisha uhamisho wake kuelekea Everton akitokea Besiktas. (Sky Sports)

PSG, Tottenham  kushindania saini ya beki wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30.

Manchester United wameanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na nyota wao, Juan Mata, Ander Herrera, Ashley Young na Daley Blind. (Mirror)

Barcelona wako tayari kutumia kiasi cha pauni milioni 140 kumsajili Philippe Coutinho kutoka Liverpool.

Ross Barkley
Chelsea wanakaribia kumsajili Ross Barkley baaa ya kupeleka ofa mpa kwa ajili ya kiungo huyo wa klabu ya Everton. (Telegraph)

Arsenal inajaribu kuhakikisha makosa ya utovu wa nidhamu ya meneja wao, Arsene Wenger yanashughulikiwa haraka ili kwenye hesabu ya mechi  atakazo fungiwa iwemo na ya FA Cup Jumapili dhidi ya Nottingham Forest.

Sunderland wanatarajiwa kumaliza usajili wa mkopo wa chipukizi wa klabu ya Liverpool, Ben Woodburn.

Jack Wilshere ataachana na uhamisho kwenda klabu za nje na badala yake abaki London ili atimize ndoto zake za kuwa shujaa wa Arsenal.

Watford wako tayari kumuuza nahodha wao, Troy Deeney na kumsajili Benik Afobe kutoka Bournemouth achukuwe nafasi yake.

Cameron Borthwick-Jackson
Klabu ya Reading inamtaka beki wa Manchester United, Cameron Borthwick-Jackson. (Daily Mail)

Celtic wanatarajiwa kukamilisha usajili wa Lewis Morgan kabla ya kumrejesha St Mirren kwa mkopo.

Liverpool wanaweza kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili Leon Goretzka baada ya uhusiano kati ya Schalke na Bayern Munich kuvunjika.

Chelsea wana uhakika wa kumsajili nyota wa klabu ya Everton, Ross Barkley kwa kiasi cha pauni milioni 15 tu. (Express)

Andy Carroll
Andy Carroll ameongezeka kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na klabu ya Chelsea mwezi Januari - anahitajika aje kusaidiana na Alvaro Morata.

Sheffield Wednesday wako kwenye mazungumzo na Jos Luhukay kutoka Uholanzi kwa ajili ya kuchukuwa nafasi ya Carlos Carvalhal kama meneja.

Mshambuliaji wa Ipswich, David McGoldrick anawindwa klabu ya Cardiff kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Chipukizi wa Nottingham Forest, Keith Asare, mwenye umri chini ya miaka 18 anawindwa na Borussia Dortmund.

Beki wa klabu ya Southampton, Sam McQueen anaweza kujiunga na Leeds, Reading au Brentford kwa mkopo.

Ryan Bertrand ana matumaini ya kuondoka Southampton mwezi huu, huku  Manchester City ikiwa mstari wa mbele kumsajili. (Sun)

Diego Simeone
Chelsea wanataka Diego Simeone achukuwe nafasi Antonio Conte kama kocha mkuu kama Muitaliano huyo ataondoka mwishoni mwa msimu.

James Tarkowski atajaribiwa na baadhi ya vilabu kuhusu kuondoka Burnley hata kama amesaini mkataba wa miaka minne na nusu .

Meneja wa West Brom, Alan Pardew ameambiwa kuwa lazima auze wachezaji kadhaa kabla ya kujaribu kusajili wapya mwezi huu. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 5 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 5 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/05/2018 02:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.