Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 19 Januari, 2018

Mesut Ozil na Jack Wilshere 
Arsenal inakaribia kuafikia makubaliano na mchezaji wa klabu hiyo, raia wa Ujerumani, Mesut Ozil na kiungo wa kati, Jack Wilshere ya kusaini mkataba mpya.

Alexis Sanchez ameambiwa afanye mazoezi na timu ya vijana, Arsene Wenger akikaribia kuwanasa Pierre-Emerick Aubameyang na Henrikh Mkhitaryan.

Swansea na Crystal Palace zinafanya tathimini juu ya kuanzisha mkakati wa kuwania saini ya beki wa Al Ahly ya Misri, Ali Maaloul. (Sun)

Everton haitawania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Leicester City, Jamie Vardy katika dirisha la usajili la mwezi Januari.
 
Jurgen Klopp amesema kuwa klabu ya Liverpool haina mpango wa kusajili wachezaji wapya. (Sky Sports)

Olivier Giroud anaweza aka mchezaji wa pili kuondoka Arsenal kwa kutumika kama sehemu ya makubaliono na Borussia Dortimund kukamilisha dili la uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang.

Emre Can
Manchester City imeonyesha nia ya kutaka kumsajili nyota wa klabu ya Liverpool, Emre Can.

Alan Pardew ameshuhudia juhudi za West Brom kumnasa Theo Walcott, Daniel Sturridge na Danny Ings zikigonga mwamba na sasa anatazamia wachezaji wa bei rahisi waje kuongeza nguvu katika safu yake ya mbele.

Swansea bado inafuatilia saini za nyota wawili wa Atletico Madrid, Kevin Gameiro na Nicolas Gaitan.

Manchester City inamrejesha mshambuliaji Larry Kayode kutoka Girona alikokuwa kwa mkopo na kumpeleka nchini Ufaransa katika klabu ya Amiens ambako anaweza kusaini mkataba wa kudumu.(Mirror)

Inter Milan iko tayari kumlipa Daniel Sturridge pauni 120,000 kwa wiki kutia msukumo katika dili la uhamisho wa mshambuliaji huyo kwa mkopo.

Leicester City inabakia kuwa na matamanio ya kumsajili beki wa Marseille, Bouna Sarr lakini inaweza kulazimika kusubiri hadi kipindi cha majira ya joto kifike.

West Brom imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya beki wa Stevenage, Ben Wilmot, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 1 licha ya kucheza mechi moja pekee kwenye Ligi Daraja la Pili. (Times)

Manchester United inakazania kuipata saini ya Alexis Sanchez kabla mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Burnley. 
(Express)

Liverpool inasita kumruhusu Danny Ings aondoke, huku mshambuliaji wao Daniel Sturridge akikaribia kuondoka Anfield.

Peter Crouch
Chelsea inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Stoke City na Uingereza, Peter Crouch baada ya kushindwa kumsajili Andy Caroll kisa majeruhi.

Arsene Wenger anasema kuwa kumpoteza Alexis Sanchez haitakuwa na maumivu sana zaidi ya ailivyokuwa kwa Robin van Persie alipojiunga na Manchester United. (Telegraph)

Manchester United iko tayari kushindana na Manchester City kuwania saini ya Jean Michael Seri kutoka Nice.

Chelsea iko hatarini kupigwa marufuku ya kusajili kwa kukiuka sheria ya usajili wa wachezaji wa kigeni walio na chini ya umri wa miaka 18. (Guardian)

Manchester United imeandaa ndege binafsi ya kumsafirsha Alexis Sanchez hadi kwenye makazi mapya.

Chelsea ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Bosnia na klabu ya Roma, Edin Dzeko na beki wa Italia, Emerson Palmieri. Uhamisho huo unakadiriwa kuweza kugharimu jumla ya pauni milioni 77.

Chelsea inaweza kuhamishia mapenzi yake kwa aliyekuwa nyota wa klabu ya Barcelona, Luis Enrique na nyota wa zamani wa 'The Blues', Juliano Belletti kumrithi Antonio Conte. (Star)

Leicester City iko tayari kuweka ofa mezani kumnasa beki wa klabu ya West Brom, Jonny Evans.

Maskauti wa klabu ya Manchester City walionekana kwenye mechi ya Lille tena siku ya Jumatano wakiendelea kumfuatilia Boubakary Soumare.

Juan Bernat
Everton imeambiwa kwamba Juan Bernat hataondoka Bayern Munich mwezi huu, klabu hiyo ikimbakisha ili asaidiane na David Alaba.

Manchester United itaanzisha mazungumzo na Marcos Rojo juu ya mkataba mpya.

Swansea City imeulizia uwezekano wa kumsajili winga wa klabu ya Ajax, Amin Younes, ambaye anatazamia kuachana na Waholanzi hao. (Daily Mail)

Alexis Sanchez amelazimika kufanya mazeozi na timu ya vijana, huku kukiwa na utata katika mpango wake kuelekea Old Trafford. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 19 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 19 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/19/2018 05:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.