Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 20 Januari, 2018

Kevin De Bruyne
Kevin De Bruyne anakaribia kusaini mkataba mpya katika klabu ya Manchester City utakaomwingizia pauni 260,000 kwa wiki.

Michael Carrick akubali kujiunga na benchi la ufundi la Manchester United atakapostaafu kucheza soka kwenye majira ya joto.

Manchester United inakumbana na changamoto kubwa kumbakisha golikipa wa Timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 20, Dean Henderson, huku klabu za Chelsea na Arsenal zikijitokeza kutaka saini ya chipukizi huyo.

Uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang kwenda Arsenal unakaribia kutimia, mkurugenzi wa Borussia Dortmund akijiandaa kukwea pipa kwenda London kukamilisha kila kitu.

Chelsea wanafanya mpango wa uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa klabu ya Crystal Palace, Christian Benteke. (Daily Mail)

Chelsea inakaribia kukamilisha taratibu za uhamisho wa mshambuliaji wa klabu ya Roma raia wa Bosinia, Edin Dzeko.

Michael Carrick atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu.

Guiso Carrilo
Klabu ya Monaco imekataa ofa ya pauni milioni 17.6 kutoka Southampton kwa ajili ya kumnasa mshambuliji wa klabu hiyo, Guiso Carrilo. (Sky Sports)

Klabu ya Burnley imekubaliana na dili la uhamisho wa kiungo wa Everton, Aaron Lennon.

Chelsea inahitaji saini za wachezaji wawili wa klabu ya Roma, Edin Dzeko na Emerson Palmeiri. (ESPN)

Pep Guardiola ndiye chaguo la kwanza la Paris Saint-Germain, klabu ya kwanza kwa matumizi makubwa ya fedha kwenye soko la usajili.

Aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United, Robin Van Persie atatambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Feyenoord siku ya Jumatatu baada ya kukubali kurejea katika klabu hiyo.

West Ham inatarajiwa kumpa Declan Rice ofa ya mkataba mpya wa miaka minne kuzifunga midomo klabu kubwa zinazowania saini ya kinda huyo.

Alexis Sanchez
Alexis Sanchez yuko kwenye kikosi cha Arsenal kitakachocheza dhidi ya Crystal Palace na anaweza kupata nafasi ya kucheza mechi ya mwisho katika dimba la Emirates kama mshambuliaji wa klabu hiyo.

Baada ya kushindwa kumnasa Theo Walcot, meneja wa klabu ya West Brom, Alan Pardew sasa anatazamia kusajili wachezaji wa bei ya chini.

Mauricio Pochettino amepewa uhuru wa kuwania saini ya Mbrazil, Malcom mwenye thamani ya pauni milioni 35 baada ya Arsenal kujiondoa kwenye kinyan'ganyiro hicho. (Mirror)

Arsene Wenger ana uhakika Jack Wilshere atabaki Arsenal - na kudokeza kwamba, nyota huyo anaweza kuwa Nahodha wa kudumu wa klabu hiyo.

Benik Afobe anatarajiwa kujiunga na Bournemouth lakini Eddie Howe anataka pauni milioni 10 kumwachia nyota huyo. (Sun)

Marco Silva anakiri kwamba Richarlison ameathiriwa na nia za Arsenal na Chelsea kutaka kumsajili. (Express)

Thibaut Courtois ameongeza orodha ya matatizo ya Antonio Conte baada ya kupata majeraha kwenye kifundo cha mguu ambayo yatamfanya akae nje ya kikosi cha Chelsea kitakachoivaa Brighton.

Swansea wamejumuisha msaada wa wakala mwenye uwezo mkubwa Jorge Mendes kuongeza nguvu kwenye mkakati wao wa kupambana kusalia katika Ligi Kuu ya Uingereza. (Telegraph)

Mauricio Pochettino amesema kuwa ni vigumu sana kwa wachezaji wa Academy ya Tottenham kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kuliko ilivyokuwa wakati alipofika katika klabu hiyo.

Jean Michael Seri
Manchester United, Manchester City kushindania saini ya kiungo wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na klabu ya Nice, Jean Michael Seri.

Chelsea iko katika hatari ya kufungiwa kusajili baada ya kukiuka taratibu za usajili wa wachezaji wa kigeni wenye umri chini miaka 18. (Guardian)

Manchester United hawatakubali Henrikh Mkhitaryan awe kikwazo kwenye dili la uhamisho wa Alexis Sanchez kutua Old Trafford.

Theo Walcott alikusanya vifaa vyake vyote katika uwanja wa mazoezi wa Arsenal mjini London. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 20 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 20 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/20/2018 12:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.