Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 13 Januari, 2018

Mohamed Salah
Florentino Perez anataka kumtumia Gareth Bale kama chambo kumnasa nyota wa klabu ya Liverpool, Mohame Salah.

Imefahamikwa kwamba, golikipa anayewindwa na Manchester United kuchukua nafasi ya David De Gea anatokea Ligi Kuu ya Uhispania, inaonekana meneja wa klabu hiyo amewatuma skauti wake kuwachunguza kwa karibu Gerónimo Rulli (golikipa wa Real Sociedad) na Jan Oblak (wa Atletico Madrid) hadi mwishoni mwa msimu huu. (Don Balon)

Winga wa klabu ya Manchester City, Leroy Sane amefichua kwamba alikataa ofa kutoka kwa Jurgen Klopp mara mbili.

Stoke City bado wana imani ya kufanikisha dili litakalomfanya Quique Sanchez Flores kuwa meneja wao mpya, licha ya mazunguzo kukwama.

Shujaa wa Manchester Utd, Ryan Giggs atafahamu kama ndiye atakayepewa kibarua cha kuinoa Timu ya Taifa ya Wales ndani ya masaa 24 yajayo.

Phil Neville anakaribia kuteuliwa kuwa meneja mpya wa Timu ya Taifa ya Uingereza ya wanawake.

Alex Pritchard aeleza jinsi David Wagner alivyomshawishi ahamie Huddersfield kutoka Norwich kwa pauni milioni 11. (Sun)

Chelsea wana matamanio makubwa ya kumfanya meneja wa klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri au meneja wa Napoli Maurizio Sarri kuwa mrithi wa Antonio Conte.

Manchester City wametoa ofa ya pauni milioni 45 kumnas mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk raia wa Brazil, Fred. (Manchester Evening News)

Arda Turan amekubali uhamisho wa mkopo kwenda klabu ya Istanbul Basaksehir kwa mkataba wa miaka miwili na nusu akitokea Barcelona.

Leicester City imekamilisha taratibu zote za uhamisho wa nyota wa klabu ya Ajaccio, Fousseni Diabate.

Naby Keita
RB Leipzig imefanya mazungumzo na Liverpool lakini hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kuhusu uhamisho wa Naby Keita. (Sky Sports)

Arsene Wenger amesisitiza kwamba, hana mpango wa kuondoka Arsenal kwenye majira ya joto na atabakia kuwa meneja hadi mwaka 2019.

Tottenham iko kwenye mazungumzo ya mikataba mipya na nyota wake wawili, Christian Eriksen na Heung-min Son.

Antonio Conte amesisitiza kwamba ataondoka Chelsea, endapo tu atafukuzwa kazi.

Manchester City wataachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez kumpa nafasi meneja wa Manchester United, Jose Mourinho.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa ataendelea kuwa meneja wa klabu hiyo hado mwaka 2019.

Chris Coleman
Meneja wa Sunderland, Chris Coleman ameiambia Watford kuwa italazimika kulipa ada ya uhamisho wa mkopo ili kufanikisha uhamisho wa Didier Ndong.

Meneja wa Birmingham, Steve Cotterill anataka kuvunja mikataba ya nyota wawili wa klabu ya Arsenal, Carl Jenkinson na Cohen Bramall wanaoichezea klabu yake kwa mkopo. (Mirror)

Rafa Benitez ana imani kuwa nahodha wa Newcastle, Jamaal Lascelles anaweza kupigania nafasi kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza kitakachoshiriki Kombe la Dunia.

Sam Allardyce amemtaka Theo Walcott aichague Everton na aachane na klabu ya Southampton aliyoichezea kabla ya kwenda Arsenal. (Express)

Jurgen Klopp alimuuza Phillippe Coutinho kwenda Barcelona kwa sababu asingekuwa na uhakika kama nyota huyo angejitoa kwa asilimia 100 kwa Liverpool.

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte anataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez mwezi Januari, akidai kwamba uhamisho huo unaweza kuwa ''uwekezaji mzuri wa pesa''.

Arsenal wanazidi kuwa na uhakika wa kuweza kumbakisha nyota wa Timu ya Taifa ya Ujerumani, Mesut Ozil. (Telegraph)

Arsene Wenger anasisitiza kwamba atabaki Arsenal hadi msimu ujao na ana matumaini ya kumbakisha Mesut Ozil pia.

Antonio Conte amekiri kwamba anaweza kuondoka Chelsea itakapfika mwisho wa msimu huu, licha ya kwamba amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa.

Sam Allardyce amemtaka Theo Walcott aondoke Arsenal ajiunge naye katika klabu ya Everton.

Javier Hernandez
Mshambuliaji wa klabu ya West Ham, Javier Hernandez hana nia ya kwenda Marekani, licha ya kwamba klabu ya Los Angeles inamhitaji.

Meneja wa West Brom, Alan Pardew amefanya mazungumzo na Jonny Evans kuhusu uhamisho wake kwenda Manchester City au Arsenal na anataka suala hilo likamilike kabla ya tarehe 28 ya mwezi Januari. (Daily Mail)

Manchester City wako tayari kuachana na jaribio lao la kumsajili Alexis Sanchez, huku klabu ya Manchester United ikionyesha nia ya kutaka kumnasa nyota huyo kutoka Chile.

Hatimaye Arsene Wenger amekiri kwamba, Alexis Sanchez hatasaini mkataba mpya katika klabu ya Arsenal lakini anaamini Mesut Ozil atakubaliana na dili jipya ambalo klabu hiyo imemwekea mezani.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anadai kwa sasa anamdharau meneja wa Chelsea, Antonio Conte. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 13 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 13 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/13/2018 07:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.