Trump anafaa kuchukuliwa hatua kali - ACT
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe |
Kwa mujibu wa taarifa ya 'The Citizen', ombi hilo lilitolewa na mkurugenzi wa kamati ya maswala ya kigeni katika chama hicho, Vennace Msebo katika taarifa.
Aliongezea: Tunapongeza hatua ya taifa la Botswana kuhusu swala hilo na tunajivunia kwamba taifa la Botswana limekuwa katika mstari wa mbele katika kushutumu kwa vitendo swala lolote linalokandamiza Afrika na watu wake.
Aidha ameyataka mataifa ya bara Afrika kutathmini matamshi hayo ya rais wa Marekani kama muamko kwa mataifa ya Afrika ili kujiimarisha kiuchumi na kukabiliana na umasikini kwa lengo la kujisimamia.
''Kwa niaba ya chama, ninashutumu pakubwa matamshi ya ubaguzi wa rangi ya rais Donad Trump. Kuwaita Waafrika na watu kutoka Afrika wachafu ni ubaguzi wa rangi na tabia ya chuki ya utawala mpya wa Marekani kwa bara Afrika na ulimwengu hautanyamaza'', alisema.
Aliongezea: Tunapongeza hatua ya taifa la Botswana kuhusu swala hilo na tunajivunia kwamba taifa la Botswana limekuwa katika mstari wa mbele katika kushutumu kwa vitendo swala lolote linalokandamiza Afrika na watu wake.
Kwa mujibu wa gazeti hilo aliongezea kwamba "vilevile tunapongeza taarifa iliotolewa na mwenyekiti wa muungano wa Afrika na hatua iliochukuliwa na mabalozi wa Afrika mjini Washington na tunaunga mkono hatu hiyo."
Aidha ameyataka mataifa ya bara Afrika kutathmini matamshi hayo ya rais wa Marekani kama muamko kwa mataifa ya Afrika ili kujiimarisha kiuchumi na kukabiliana na umasikini kwa lengo la kujisimamia.
Trump anafaa kuchukuliwa hatua kali - ACT
Reviewed by Zero Degree
on
1/13/2018 08:02:00 PM
Rating: