Loading...

Rais Magufuli akataa kutawala miaka 7


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameweka wazi kuwa hana mpango wowote wa kuongeza muda wa kukaa madarakani kutoka miaka 5-7 na pia hafurahishwi na mijadala hiyo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Januari 13 wakati alipokutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi IKulu, ndg. Humphrey Polepole na kumtuma awajulishe watanzania na wana CCM kwamba wapuuze mijadala hiyo kwani jambo hilo halijawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama.

Kupitia taarifa iliyotlewa na Ikulu, Rais Magufuli amemuagiza Polepole kuwajulisha watanzania na wana CCM kuwa wasikubali kuyumbishwa au kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi na badala yake wajielekeze katika kukuza uchumi na kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2017.

Mjadala wa kuhusu kuongeza muda wa uongozi uliibuka pale Mbunge Kondoa Juma Nkamia alipoweka wazi hisia zake za kupeleka mjadala bungeni wa kutengeneza muswada utakaojadili viongozi wanaochaguliwa kukaa madarakani kwa miaka 7 badala ya mitano iliyopo sasa.

Soma taarifa kamili hapo chini:


Rais Magufuli akataa kutawala miaka 7 Rais Magufuli akataa kutawala miaka 7 Reviewed by Zero Degree on 1/13/2018 08:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.