Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 23 Januari, 2018

Pierre-Emerick Aubameyang
Klabu ya Borussia Dortmund inamtaka Olivier Giroud kama sehemu ya ada ya uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang - kama sivyo, itaahirisha kummuza nyota huyo hadi kwenye majira ya joto.

Chelsea imekubali kulipa kiasi cha pauni milioni 50 kuwanasa nyota wawili wa klabu ya Roma, Edin Dzeko na Emerson Palmieri.

Mbio za Arsenal na Tottenham kuwania saini ya winga wa PSG zimechochewa na kauli ya mchezaji huyo, ambaye amedai anataka kuondoa nchini Ufaransa.

West Ham haitamruhusu Javier Hernandez kuondoka mwezi January baada ya kugundua kwamba Andy Carroll atakuwa nje ya kikosi kwa miezi mitatu na Manuel Lanzini kuwa nje kwa wiki sita. (Mirror)

Kwa mujibu wa taarifa ya meneja mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta, klabu hiyo ya Italia inaweza kushindwa kufanikisha uhamisho wa nyota wa Liverpool, Emre Can. 

Alvaro Morata na Cesc Fabregas wataukosa mechezo wa michuano ya Carabao kati ya Arsenal na Chelsea.

Sunderland inafanya mazungumzo na klabu ya Wolves juu ya uhamisho wa winga wa klabu hiyo, Ben Marshall.

Aaron Lennon
Aaron Lennon amekamilisha uhamisho wake kwenda Burnley kwa kusaini kandarasi ya miaka mitatu na klabu hiyo akitokea everton. (Sky Sports)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu yake iko katika mazungumzo na Borussia Dortmund juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ta taifa ya Gabon Pierre-Emelic Aubameyang.

Uhamisho wa Alexis Sanchez umeonyesha kwamba suala la umri sio tija tena, kwenye soko la usajili wa wachezaji kwa sasa. (ESPN)

Newcastle inafanya mpango wa kukamilisha dili la uhamisho wa mshambuliaji wa Atletico Madrid, Kevin Gameiro.

Chelsea imempa Edin Dzeko ofa ya mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya pauni milioni 7 ili arejee kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Kiungo wa klabu ya Newcastle, Jonjo Shelvey anakaribia kujiunga na West Ham kwa dau la pauni milioni 12.

Moussa Dembele anatazamia kuondoka Celtic mwezi huu. (Express) 

Manchester City inamtaka nyota wa klabu ya Athletic Bilbao, Aymeric Laporte na inafikiria kuhusu uwezekano wa kulipa dau la pauni milioni 60.

Lassana Diarra 'Lass'
Lassana Diarra anakaribia kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain kwa uhamisho wa kushitukiza. (Sun)

Baada ya kuwasili Manchester United, Alexis Sanchez ameishauri klabu hiyo imsajili beki wa kati wa klabu ya Barcelona, Samuel Umtiti. 

Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez tayari ana orodha ya mwihso ya majina matatu yanayotegemewa kurithi  nafasi Zinedine Zidane.

Cristiano Ronaldo amedai nyota wa klabu ya Barcelona, André Gomes kuwa ndiye anayefuata kwenye orodha ya wachezaji wa klabu hiyo watakaoondoka kwenye majira ya joto. (Don Balon)

Mkurugenzi wa kandanda wa klabu ya Roma, Ramón Rodríguez Verdejo '
Monchi' amesema kwamba klabu hiyo inaweza kufukiria uwezekano wa kumnasa nyota wa klabu ya Liverpool, Daniel Sturridge kama Edin Dzeko atauzwa.

Wolves imejiunga na West Brom kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Bournemouth, Benik Afobe.

West Brom itaachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Watford, Troy Deeney kama Jonny Evans hataondoka mwezi huu.

Leeds inafanya mpango kutoa ofa ya pauni milioni 7 kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa, Ross McCormack.

Charlton inatarajiwa kumsajili winga wa klabu ya Crystal Palace, Sullay Kaikai na kiungo wa Wolves, Michael Zyro kwa mkopo. (Star)

Kenedy
Newcastle inatarajiwa kufanikisha uhamisho wa winga wa klabu ya Chelsea, Kenedy kwa mkopo ndani ya masaa 24 yajayo.

Crystal Palace inakaribia kukamilisha uhamisho wa beki wa klabu ya Zaglebie Lubin, Jaroslaw Jach kwa pauni milioni 2. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa klabu ya West Ham, Andy Carroll atakuwa nje ya kikosi cha klabu hiyo ya Uingereza kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu uliovunjika. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 23 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 23 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/23/2018 05:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.