Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 21 Januari, 2018

Wilfried Zaha
Tottenham na Arsenal zinashindania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha.

Klabu ya Juventus inataka kumsajili nyota wa Arsenal, Jack Wilshere kama mchezaji huru kwenye majira ya joto.

Tottenham inajaribu kwa mara ya mwisho kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Kevin Gameiro.

Mipango klabu ya Arsenal iliyofanyika kwa siri kumnasa Luke Shaw imekumbana na kikwazo baada ya Manchester United kukataa kumuuza mchezaji huyo wakati wa mazungumzo yao juu ya uhamisho wa Alexis Sanchez.

Sunderland ina mapango wa kumsajili chipukizi wa klabu ya Chelsea, Ethan Ampadu kwa mkopo. (Sun)

Arsenal inaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang - kama imejiandaa kulipa dau la pauni milioni 55.

Matumaini ya Daniel Sturridge kujiunga na klabu ya Inter Milan yako hatarini baada ya Liverpool kudai dau la pauni milioni 30. (Express)

Jose Mourinho anasema kuwa Alexis Sanchez anakaribia kumaliza taratibu za uhamisho wake kwenda Manchester United, huku Arsene Wenger akimsubiri Henrikh Mkhtaryan. 

Arsenal imejitosa kwa mara ya kwanza kutoa ofa kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang (ESPN)

Fred
Manchester City imefanya mazungumzo na klabu ya Shakhtar Donetsk juu ya uhamisho wa kiungo wa klabu hiyo, Fred, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 40. (Telegraph)

Uongozi wa klabu ya Manchester City ulifanya kikao kabla ya ushindi wao dhidi ya Newcastle, huku klabu hiyo ikiwa kwenye mbio za kuwania saini ya Fred na Jonny Evans.

Samir Nasri anatarajiwa kurejea katika Ligi Kuu ya Uingereza, safari klabu ya West Ham ikiwa ndiyo inawania saini ya kiungo huyo wa Antalyaspor.

Liverpool ina fanya mpango wa uhamisho wa Daniel Sturridge kwenda Inter Milan mwezi huu kwa kuwazui uhamisho wa Danny Ings na Ben Woodburn.

Everton imeendelea kufuatilia saini ya beki wa klabu ya Chelsea, Baba Rahman na Patrick van Aanholt wa 
 Crystal Palace.

Newcastle United imeuliza kama kuna uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Everton, Sandro Ramirez kwa mkopo.

Dili la uhamisho wa Alexis Sanchez limekamilika baada ya Manchester United kukubali kumwacha Mkhitaryan ajiunge na 'The Gunners'.

Klabu ya Borussia Dortmund imemweka sokoni Andre Schurrle kwa klabu yoyote itakayokuwa tayari kusajili nyota huyo kwa mkopo, huku klabu hiyo ikiwa tayari kuendelea kulipa nusu ya mshahara wa mchezaji huyo wa pauni 150,000 kwa wiki.

Edin Dzeko na Emerson Palmieri
Edin Dzeko na Palmieri wanakaribia kujiunga na Chelsea baada ya klabu hiyo kukubali kulipa jumla ya pauni milioni 44 kwa ajili ya uhamisho wa wawili hao kutoka Roma.

Klabu ya West Brom imekataa ofa ya pauni milioni 4 kutoka Leeds kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji wao, Tyler Roberts, ambaye anaweza kujiunga na klabu ya Rangers au Marseille kwa sasa. (Daily Mail)

Arsenal na Liverpool zimepata pigo kubwa katika dirisha la usajili la mwezi huu baada ya nyota wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar kudai kuwa mpango wake ni kujiunga na Barcelona.

Paul Pogba ataomba mshahara wake uongezwe mara mbili hadi pauni 400,000 kwa wiki ili alingane na Alexis Sanchez.

Roma imejiunga na klabu ya AC Milan pamoja na Valencia kwenye mbio za kuwania saini ya mchezaji wa Manchester United, Matteo Darmian - lakini klabu hiyo ya Uingereza haiko tayari kumwachia mchezaji huyo aondoke moja kwa moja bali kwa uhamisho wa mkopo. (Mirror)

Valencia inafanya mpango wa kumnasa nyota wa klabu ya Manchester United, Juan Mata kwenye majira ya joto wakati mkataba wake utakapoisha.

Arsenal inafanya mpango wa kumsajili nyota wa klabu ya PSG, Lucas Moura kurithi nafasi ya Alexis Sanchez.

Jonny Evans
Arsenal inaweza kuanzisha mkakati wa kumsajili Jonny Evans kwa sababu klabu ya West Brom inaweza kupoteza pauni milioni 20 kama haitamuuza mchezaji huyo mwezi huu. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 21 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 21 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/21/2018 12:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.