Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 28 Januari, 2018

Antonio Conte na Michy Batshuayi
Antonio Conte anadai hana uhakika kama Michy Batshuayi atabaki Stamford Bridge endapo klabu ya Chelsea itaamua kusajili mshambuliaji mwingine mwezi Januari.

Diafra Sakho anakaribia kujiunga na klabu ya Rennes akitokea West Ham kwa uhamisho utakaogharimu pauni milioni 8. (Sky Sports)

Edison Cavani ameivunja rekodi ya Zlatan Ibrahimovic katika klabu ya PSG kwa kuwa mshambuliaji mwenye magoli mengi baada ya kufanikiwa kuifungia klabu hiyo katika mechi yao dhidi ya Montpellier na kufikisha magoli 157.

Klabu ya Monaco imefanikiwa kumnasa chipukizi wa klabu ya Genoa, Pietro Pellegri na kuipiku Juventus. (ESPN)

Klabu ya Manchester City iko tayari kutoa ofa ya pauni milioni 150 kumnasa mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard.

Manchester United wako makini kufuatilia mipango ya klabu ya Borussia Dortmund na nyota wao, Marc Bartra, huku kukiwa na uvumi kwamba klabu hiyo ina mpango wa kumuuza beki huyo.

Mauricio Pochettino ni kinara kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa na klabu ya Real Madrid - kwa sababu ya uwezo aliouonyesha kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa na Tottenham.

Daniel Sturridge
Daniel Sturridge anatarajiwa kuhamia Inter Milan - baada ya klabu ya Liverpool kupunguza ada ya uhamisho wa nyota huyo. (Mirror)

Siri ya rais wa Real Madrid, Florentino Perez na Neymar kuhusu uhamisho wa Mbrazil huyo inamhusisha Cristiano Ronaldo katikati.

Diego Simeone alikua na mpango wa kumsajili winga wa klabu ya PSV na timu ya taifa ya Mexico, Hirving Lozano katika kipindi cha majira ya joto kilichopita.

Messi ameishauri klabu ya Barcelona kuongeza nguvu kikosini kwa  kumnasa nyota wa Real Madrid, huku kukiwa na ripoti zinazodai kuwa Marco Asensio ndio nyota pekee ambaye Mwajentina huyo anamkubali. (Don Balon)

Chelsea wanajiandaa kumpa kibarua Luis Enrique achukue nafasi ya Antonio Conte kwenye majira ya joto.

Burnley inamtaka beki wa klabu ya Arsenal, Rob Holding kwa mkopo kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia.

Mstakabali wa maisha ya Michael Keane katika klabu ya Everton uko shakani, huku meneja wa klabu hiyo, Sam Allardyce akiwa na mpango wa kumuuza nyota huyo mwezi huu au kwenye majira ya joto.

Newcastle ina nafasi kubwa kumnasa raia wa Brazil, Luan mbele ya klabu ya Liverpool.

Inawezakana muda wa Benik Afobe katika klabu ya Bournemouth unaelekea mwishoni baada ya nyota huyo kujikuta anatofautiana na meneja wake, Eddie Howe kisa kikidaiwa kuwa nia kalamu. (Sun)

Ripoti zinadai kwamba ofa ya klabu ya Liverpool kumnasa golikipa wa Roma, Alisson Becker ilikataliwa.

Matteo Darmian
Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anatarajiwa kuzikataa ofa kutoka AS Roma na Juventus kwa ajili ya uhamisho wa Muitaliano, Matteo Darmian kwa mkopo. (Express)

Chelsea imekataa ofa ya klabu ya Real Madrid, ambayo inaambatana na kubadilishana Eden Hazard kwa Cristiano Ronaldo.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp anafirikia kumsajili winga wa klabu ya Monaco, Keita Balde, huku klabu ya Arsenal ikiwa na nia ya kumsajili nyota huyo.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amekanusha kujitokeza kutaka saini ya mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang.

Manchester United na Manchester City zinatarajiwa kuingia katika ushindani kwa mara nyingine tena wiki hii - safari hii ikiwa ni kwa kiuongo wa Brazil, Fred.

Tottenham ina uhakika wa kuipiku klabu ya Bayern Munich katika mbio za kuwania saini ya Mbrazil, Lucas Moura.

Jack Harrison
Middlesbrough iko mstari wa mbele katika mbio za kuwania saini ya winga wa klabu ya New York City, Jack Harrison. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 28 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 28 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/28/2018 12:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.