Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 3 Januari, 2018

Sergio Aguero
Sergio Aguero anasema kuwa angependelea kusalia katika klabu ya Manchester City hadi 2020, ambapo mkataba wake utakuwa umemalizika.

Arsenal iko kwenye mazungumzo na klabu ya PAS Giannina kuhusu uhamisho wa beki wa klabu hiyo, Konstantinos Mavropanos, ambaye ana umri wa miaka 20 kwa sasa. (Sky Sports)

Antonio Conte anasema kwamba, David Luiz na Michy Batshuayi wanaweza kuondoka Chelsea mwezi Januari kama watapenda. (Telegraph)

Cenk Tosun 
Everton watajaribu kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Besiktas, Cenk Tosun leo hii katika mkutano wao na rais wa klabu hiyo, Fikret Orman. (Guardian)

Philippe Coutinho amesema ameichezea Liverpool mechi ya mwisho na kwa sasa atakazania uhamisho wake kuelekea Barcelona ukamilike mwezi huu. (Express)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amekanusha taarifa zinazodai kuwa klabu yake  imemsajili beki wa Juventus, Giorgio Chiellini mwezi Januari.

Klabu ya West Ham iko tayari kulipa pauni milioni 15 kufanikisha uhamisho wa nyota wa Timu ya Taifa ya Wales, Joe Allen kutoka Stoke City. (Daily Mail)

Pep Guardiola amethibitisha kwamba, mshambuliaji wa Manchester City, Gabriel Jesus atakuwa nje kwa muda wa wiki nne hadi sita kwa sababu ya majeraha kwenye goti.

Alex Sandro
Chelsea wako tayari kutoa pauni milioni 50 mwezi Januari ili kumnasa beki wa kalbu ya Juventus, Alex Sandro.

Arsene Wenger amefungua milango kwa Alexis Sanchez mwezi huu endapo Arsenal itapata mbadala wa nyota huyo. (Mirror)

Aston Villa, Middlesbrough, Fulham na Derby zinamtamani aliyekuwa kiungo wa Manchester City, Abdisalam Ibrahim, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Valarenga.

Klabu ya Watford ina matamanio makubwa ya kumsajili golikipa wa Getafe, Vicente Guaita.

Norwich wamempa mkataba mrefu kiungo mwenye asili ya kijerumaniwill, Tom Trybull.

QPR wanamtaka mshambuliaji wa klanu ya Peterborough, Jack Marriott kwa kubadilishana na Conor Washington. (Star)

Lucas Moura
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ana matamanio makubwa ya kumsajili winga wa PSG, Lucas Moura kwa mkopo mwezi Januari. (Sun)

Brendan Rodgers amekiri kwamba ana mpango wa kumtoa Eboue Kouassi kwa mkopo katika kipindi kilichosalia kabla ya kumalizika kwa msimu huu. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 3 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 3 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/03/2018 05:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.