Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 10 Januari, 2018

Kiungo wa Real Madrid, Isco akiwa na meneja wa timu hiyo, Zinedine Zidane mzoezini
Zinedine Zidane anasisitiza kwamba klabu ya Real Madrid haihitaji wachezaji wapya na kudai kwamba waliopo wanajitosheleza.

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amekiri kuwa klabu yake ilikuwa ikuwania saini ya beki wa Southampton, Virgil Van Dijk.

Klabu ya Sevilla ina matamanio makubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi kwa mkopo.

Christensen amesaini mkataba mpya na klabu ya Chelsea utakaomfanya akae Stamford Bridge hadi mwaka 2022. (ESPN)

Everton wako mstari wa mbele kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya winga wa klabu ya Arsenla, Theo Walcott kwa dau la pauni milioni 20.

Klabu ya Barcelona tayari imewaweka sokoni Arda Turan, Aleix Vidal, Gerard Deulofeu, Paco Alcacer, Jose Arnaiz, Andre Gomes, Denis Suarez na Javier Mascherano. (Daily Mail)

Stoke City wamewasiliana na meneja wa timu ya taifa ya Ireland, Martin O'Neill, ikiwa nia katika harakati za kutafuta meneja mpya wa klabu yao.

Antonio Valencia anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha Manchester United  kwenye mechi dhidi ya Stoke City.

Steve Bruce
Meneja wa Aston Villa, Steve Bruce ana matumaini ya kuwasajili nyota wawili wa Leicester, Leonard Ulloa na Daniel Amartey kwa mkopo. (Telegraph)

Chelsea hawatakubali ofa yoyote kutoka Crystal Palace kwa ajili ya usajili wa kiungo wao, Ruben Loftus-Cheek kwa mkataba wa kudumu.

Bournemouth wamekataa ofa ya pauni milioni 5 kutoka West Ham kwa ajili ya Harry Arter.

Brighton wanaandaa ofa ya pauni milioni 3 kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu ya Aston Villa, Keinan Davis.

Huddersfield wanakaribia kukamilisha taraibu za usajili wa kiungo wa Norwich City, Alex Pritchard kwa pauni milioni 11. (Sun)

Thomas Lemar
Monaco wametangaza bei ya chini ya pauni milioni 90 kuwa kianzio kwa klabu itakayomhitaji Thomas Lemar mwezi hii au kwenye majira ya joto.

Southampton wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 19 kwa ajili kiungo wa Atletico Madrid, Nicolas Gaitan lakini wanakumbana na ushindani kutoka klabu ya Crystal Palace na Everton.

Arsenal wanajiandaa kuanzisha mazungumzo na Jack Wilshere na wanaweza kumpa ofa ya mshahara wa kawaida lakini watamuongezea bonasi ambazo zitategemeana na kiwango chake. (Mirror)

Manchester City wametoa ofa ya pauni milioni 20 ili kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsena, huku mshambuliaji huyo wa Chile andaiwa kukubali mshahara wa pauni 250,00 kwa wiki. (Guardian)

Kwa mujibu wa ripoti za Uhispania, Real Madrid wamepokea ofa ya pauni milioni 84 kutoka kwa klabu ambayo haijajulikana hadi sasa kwa ajili uhamisho wa nyota wao Gareth Bale. (Star)

Boca Juniors wamekanusha kupokea ofa kutoka Arsenal kwa ajili ya Cristian Pavon, mchezaji ambaye washika bunduki hao wanamchukulia kama mtu sahihi anayefaa kuchukuwa nafasi ya Alexis Sanchez.

Andrea Belotti
Mshambuliaji wa Torino, Andrea Belotti ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaowaniwa na klabu ya Manchester United kuchukuwa nafasi ya Zlatan Ibrahimovic.

Barcelona wako kwenye mazungumzo na klabu ya Istanbul Basaksehir kuhusu uhamisho wa kiungo wao, Arda Turan. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 10 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 10 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/10/2018 01:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.