Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 24 Januari, 2018

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann
Meneja wa klabu ya Barcelona, Ernesto Valverde anataka kumtumia mchezaji mkubwa wa klabu hiyo kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann. (Don Balon)

Arsenal iko kwenye nafasi nzuri kukamilisha uhamisho wa Jonny Evans pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang, ambao utaigharimu klabu hiyo kiasi cha pauni milioni 75.

West Ham inafikiria kuhusu kutoa ofa kwa ajili ya uhamisho wa kiungo wa klabu ya Real Betis, Fabián Ruiz baada ya David Moyes kumchunguza mchezaji huyo wakati akicheza dhidid ya Barcelona. (Telegraph)

Klabu ya Feyenoord imeikataa ofa ya klabu ya Newcastle United kumnasa mshambuliaji wa klabu hiyo ya Uholanzi, Nicolai Jorgensen.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anasema kuwa kwa sasa matumaini yake makubwa yako kwenye michuano ya Carabao.

West Brom ina matamanio makubwa ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Bournemouth, Benik Afobe.

Martin O'Neill amesaini mkataba mpya kuendelea kuinoa timu ya taifa ya Ireland hadi mwaka 2020.

Antonio Conte amekanusha taarifa ziliodai kwamba alikuwa na nia ya kumsajili Alexis Sanchez kabla hajakubali kujiunga na Manchester United. (Sky Sports)

Andre Schurrle
Klabu ya West Brom inamvizia kiungo wa klabu ya Borussia Dortmund, Andre Schurrle kwa mkopo. (Times)

Arsenal imeongeza ofa yao kumnasa mshambuliaji wa Borussia Dortmund hadi kufikia pauni milioni 50.9.

West Ham imefanya mazungumzo zaidi na klabu ya Inter Milan juu ya usajili wa kiungo wao na raia wa Ureno, Joao Mario.

West Brom iko msatari wa mbele kukamilisha dili la uhamisho wa beki wa kati wa Zamalek, Ali Gabr kwa mkopo.

Newcastle imeendelea kumfanyia uchunguzi mshambuliaji wa Leicester City, Islam Slimani mwenye thamani ya pauni milioni 20, wakati huo huo Benitez ameulizia kuhusu uhamisho wa mkopo wa Sandro Ramirez kutoka Everton.

Bournemouth, West Ham, Crystal Palace na Newcastle zitamchunguza beki wa klabu ya Dundee, Jack Hendry akicheza dhidi ya Hibernian Jumatano usiku.

Aston Villa ina matumaini ya kukamilisha uhamisho wa beki wa Manchester United, Axel Tuanzebe kwa mkopo wikendi ijayo. (Daily Mail)

Almamy Toure
Baada ya kumkosa Bouna Sarr wa Marseille, klabu ya Leicester City inageukia kwa beki wa Monaco, Almamy Toure.

Chipukizi wa klabu ya Stoke City, Harry Souttar amesaini mkataba mpya na kundoka kwenda Ross County kwa mkopo.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anamtaka kiungo wa klabu ya Nice raia wa Ivory Coast, Jean Michael Seri.

Swansea inampa Nicolas Gaitan ofa ya mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki aondoke Atletico Madrid na kujiunga na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza inayopigana kuondokana na adha ya kushuka daraja. (Sun)

Chelsea iko tayari kumjumuisha Edin Dzeko kwenye kikosi chao cha kwanza, huku kukiwa na wasiwasi juu ya kiwango cha nyota anayeshirikiria rekodi ya usajili ya klabu hiyo, Alvaro Morata.

West Ham imelazimika kufanya mabadiliko kwenye mipango yao ya usajili baada ya Marko Arnautovic na Manuel Lanzini kupata majeraha.

Watford itampa Richarlison ofa ya mkataba mpya wenye maslahi mazuri, ikiwa ni mpango wa kujaribu kumshawishi abaki chini ya meneja mpya wa klabu hiyo, Javi Gracia. (Star)

Raheem Sterling atakuwa mchezaji mwingine wa Manchester City kupewa mkataba mpya hivi karibuni.

Louis van Gaal ametajwa kwenye orodha ya makocha wanaotarajiwa kupewa kibarua cha kuinoa Australia kwenye Kombe la Dunia.

Santi Cazorla
Kiungo wa klabu ya Arsenal, Santi Cazorla anatarajia kurejea dimbani mwaka ujao, wakati huu akiwa anaendelea kuuguza majeraha yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu.

Everton iko kwenye mazungumzo na mkurugenzi wa kandanda wa PSV, Marcel Brands juu ya kazi mpya Goodison Park.

Nottingham Forest ina nia ya kumsajili golikipa wa klabu ya Bournemouth, Adam Federici. (Daily Mirror)

Rangers inahofia kumkosa Ryan Jack kwa kipindi chote cha msimu huu ambacho kimesalia baada ya kupata majeraha kwenye goti.

Bolton, Barnsley na Millwall zimejiunga na klabu ya Aberdeen kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa Hibernian, Dylan McGeough, ambaye mkataba wake unamalizika kwenye majira ya joto. (Record)

Meneja wa Celtic, Brendan Rodgers anakiri kwamba, atalazimika kurejea kwenye soko la usajili wa wachezaji kusaka mshambuliaji mwingine kama Moussa Dembele ataondoka mwezi huu. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 24 Januari, 2018  Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 24 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/24/2018 01:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.