Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 31 Januari, 2018

Neymar
Rais wa La Liga, Javier Tebas amemtaka nyota wa klabu ya PSG, Neymar arejee Uhispania.

Mauricio Pochettino anaamini kuwa kumsajili Lucas Moura ni wasaa mzuri sana kwa klabu ya Tottenham.

Michy Batshuayi anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Borussia Dortmund kwa muda miezi 6 akitokea Chelsea.

Nyota wa klabu ya Bournemouth, Harry Arter ameambiwa hawezi kuondoka katika klabu hiyo hadi kwenye majira ya joto.

Meneja wa Sunderland, Chris Coleman anafanya mpango wa kumsajili straika wa klabu ya Sheffield Wednesday, Jordan Rhodes kwa mkopo. (Sun)

Neymar amesema kuwa kitendo cha Lucas Moura kulazimishwa kuondoka PSG hakikuwa cha haki.

Wakala wa Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa mteja wake anafikiri kujiunga na Ligi ya MLS.

Mesut Ozil amesaini mkataba mpya na klabu ya Arsenal utakaomfanya aendelee kutumikia klabu hiyo hadi mwaka 2021.

Pep Guardiola amesema kuwa ni vigumu sana kwa Manchester City kukamilisha uhamisho wa Riyad Mahrez kablya dirisha la usajili halijafungwa. (ESPN)

Klabu ya Chelsea imemruhusu Michy Batshiayi aondoke kwenda Borussia Dortmund kwa mkopo.

Arsene Wenger akiwa na mchezaji wake mpya Aubameyang
Klabu ya Arsenal imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre Emerick Aubameyang kwa dau la pauni milioni 60.

Beki wa klabu ya Burnley, Tom Anderson anajiunga Doncaster kwa mkopo.

Rolando Aarons ameachana na uhamisho wa kwenda Hull City kwa mkopo, na badala yake ameichagua klabu ya Hellas Verona.

Klabu ya Swansea inakaribia kumnasa nyota wa klabu ya West Ham, Andre Ayew. (Sky Sports)

Beki wa Manchester United, Daley Blind anatarajiwa kujiunga na klabu ya Roma kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili saa tano usiku.

Beki wa klabu Arsenal, Mathieu Debuchy yuko kwenye mazungumzo na klabu yake akiomba mkataba wake uvunjwe ili ajiunge na Saint-Etienne.

Napoli imetoa ofa ya kumsajili kiungo wa klabu ya Everton, Davy Klaassen kwa mkopo kwa kipindi kilichosalia kabla ya kumalizika kwa msimu huu.

Lazar Markovic
Klabu ya Wolfsburg inafanya mpango wa kumsajili Lazar Markovic kutoka Liverpool.

Newcastle United ina matumaini ya kumsajili golikipa wa Sparta Prague, Martin Dubravka kwa mkopo. (Daily Mail)

Chelsea inakaribia kumnasa Olivier Giroud kwa pauni miloni 18, ambapo usajili huo utatoa nafasi kwa Pierre-Emerick Aubameyang kujiunga na klabu ya Arsenal na Michy Batshuayi kwenda Borussia Dortmund kwa mkopo.

Swansea City inatarajia kuvunja rekodi yao ya usajili kumrejesha Andre Ayew kikosini kwa pauni milioni 18.

Klabu ya Newcastle inafanya mpango wa kumnasa Eliaquim Mangala pamoja na Islam Slimani.

Crystal Palace inakaribia kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Preston, Jordan Hugill kwa pauni milioni 8. (Telegraph)

Manchester City italazimika kulipa kiasi cha pauni milioni 70 kumnasa nyota wa klabu ya Leicester City, Riyad Mahrez kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili saa tano usiku.

Barnsley imetoa ofa ya pauni 350,000 kwa ajili ya usajili wa golikipa wa klabu ya Oxford, Simon Eastwood.

Bristol City inahitaji dau la pauni milioni 10 ili kumruhusu beki wao, Aden Flint aondoke. (Star)

Klabu ya Roma iko kwenye mawasilisano na Manchester United juu ya uhamisho wa beki wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Uholanzi, Daley Blind.

West Ham inaendele kubakia na nia yao ya kwasajili Morgan Schneiderlin wa Everton na Joe Allen Stoke City, wakati David Moyes akitarajiwa kutoa ofa kwa ajili ya uhamisho wa James Maddison kutoka Norwich. (Mirror)

Rafa Benitez
Rafa Benitez alifanya mazungumzo na mmiliki wa klabu ya Newcastle, Mike Ashley siku ya Jumanne, huku muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili ukuzidi kuyoyoma.

Celtic inaweza kumsajili Scott Bain na kutatu shida ya golikipa baada ya ofa yao kumnasa Trevor Carson wa Motherwell kukataliwa. (Express)

Chelsea imekubali kulipa dau la pauni milioni 18 kwa ajili ya uhamisho wa Oliver Giroud kutoka Arsenal.

Klabu ya Arsena inatarajiwa kukamilisha usajili wa nyota wa klabu ya Shalke 04, Max Meyer kabla dirisha la usajili halijafungwa.

Mipango ya klabu ya Southampton kuvunja rekodi kwa kumnsa nyota wa klabu ya Spartack Moscow, Quincy Promes imegonga mwamba.

Riyad Mahrez ameomba uhamisho wake ushughulikiwe, lakini klabu ya Leceister City inahitaji kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa Manchester City. (talkSport)

Manchester City iko tayari kumruhusu Tosin Adarabioyo aondoke kwa mkopo, huku klabu ya Sheffield Wednesday ikionyesha nia ya kutaka kumsajili nyota huyo. (Times)

Celtic inabaki na matamanio ya kumnasa golikipa wa Arsenal, Emiliano Martinez wakiwa na hamu ya kuwa na magolikipa wa kutosha kikosini. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 31 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 31 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/31/2018 09:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.