Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 22 Januari, 2018
Eden Hazard |
Eden Hazard anaamini kwamba, klabu ya Chelsea ina washambuliaji wa kutosha na hakuna haja ya kusajili wengine, huku kukiwa na uvumi kwamba klabu hiyo inatarajiwa kuongeza wachezaji wapya kikosini.
Liverpool itamruhusu mshambuliaji wake, Daniel Sturridge kuondoka Anfield katika dirisha la usajili la mwezi huu.
Klabu ya Lile inategemea kupokea ofa kutoka Manchester City kwa ajili ya uhamisho wa kiungo, Boubakary Soumare. (Sky Sports)
Klabu ya Lile inategemea kupokea ofa kutoka Manchester City kwa ajili ya uhamisho wa kiungo, Boubakary Soumare. (Sky Sports)
Robin Van Persie amerejea katika klabu ya Feyenoord miaka 14 tangu anunuliwe na klabu ya Arsenal, alipokuwa na umri wa miaka 20.
Jurgen Klopp anasisitiza kwamba hawezi kumruhusu mechezaji wa Liverpool ajiunge na timu pinzani katika ya msimu kama ilivyofanya Arsenal.
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na Manchester City, Mario Baloteli anakaribia kukubali uhamisho wake kama mchezaji huru kwenda Juventus kwa mkataba wa miaka mitano.
Liverpool na Arsenal zimeliweka kiporo suala la uhamisho wa winga wa Monaco, Thomas Lemar hadi kwenye majira ya joto, lakini zinaweza kukumbana na ushindani mkubwa toka kwa Atletico Madrid katika kuwania saini ya nyota hyo mwenye thamani ya pauni milioni 90.
Alexis Sanchez ameonekana akipiga picha akiwa amevaa jezi ya Manchester United katika dimba la Old Traford baada ya kufanyiwa vipimo, huku akisubiri kukamilika kwa dili lake la uhamisho.
Arturo Vidal |
Arturo Vidal ameeleza kwamba ataondoka Bayern Munich wakati Leon Gortzeka atakapowasili katika klabu hiyo. (Daily Mail)
Manchester City waliachana na suala la kumfuatilia Alexis Sanchez ili wapate fursa ya kumfuatilia Mbrazil, Fred kwa karibu.
Baada ya kufeli kwa Thomas Lemar, Liverpool sasa wanataka kumsajili Christian Pulisic kutoka Marekani.

Manchester United wanakumbana na ushindani kutoka klabu kadhaa kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa Real Madrid, Gareth Bale. (Star)
Meneja wa Everton, Sam Allardyce amekiri kwamba uwezekano wa kushaka daraja msimu huu bado upo. (Express)
Roma tayari ina mipango ya kuziba pengo la Dzeko na Emeron iwapo wawili hao watajiunga na Chelsea mwezi huu.
Mauricio Pochettino amesema Tottenham haina mpango wa kumfuatilia winga klabu ya Bordeaux, Malcolm.
Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amekiri kuwa Mitchy Batshuayi huenda akaondoka mwezi Januari. (Goal)

Klabu ya Bayern Munich imetoa ofa ya zaid ya pauni milioni 100 kumsahwishi nyota klabu ya Real Madrid, Gareth Bale akubali kuhamia Ujerumani.
Christiano Ronaldo ameweka wazi kuwa anataka mazungumzo na klabu hiyo juu ya mkataba mpya kabla hajachukuwa uamuzi wa kuondoka, na kuonya kwamba kuondoka kwake kunaweza kupelekea wachezaji kadhaa wa muhimu kuachana na klabu hiyo. (Don Balon)
Meneja wa klabu ya Roma, Eusebio Di Francesco ameiambia Chelsea kuwa Edin Dzeko ni mchezaji muhumu sana katika kikosi chake, huku kukiwa na uvumi mkubwa unaoendelea kumhusisha nyota huyo na uhamisho kwenda Stamford Bridge. (ESPN)
Arsene Wenger amesema kuwa, sintofahamu inayozunguka maisha ya Alexis Sanchez katika klabu ya Arsenal imeathiri morali ya wachezaji wake.
Arsene Wenger amesema kuwa, sintofahamu inayozunguka maisha ya Alexis Sanchez katika klabu ya Arsenal imeathiri morali ya wachezaji wake.
Sam Allardyce ameeleza kwamba suala la Wayne Rooney na Gylfi Sigurdsson kuwa katika timu mmoja haliwezekani kwasababu ya ukosefu wa nafasi katika kikosi. (Guardian)
Daniel Sturridge amaeiambia Liverpool anataka kujiunga na Sevilla baada ya klabu hiyo ya Uingereza kukataa uhamisho wake kwa mkopo.
Daniel Sturridge |
Arsene Wenger amesisitiza kwamba suala zima la fedha ndio chanzo kikubwa cha uhamisho wa Alexis Sanchez kwenda Manchester United.
Everton, Newcastle na Brighton zinawania saini ya beki wa Bristol City, Joe Bryan anayekadiriwa kuwa na thamani pauni milioni 7. (Mirror)
Rafael Benitez ameiambia Newcastle kuwa atafanya mazungumzo yanayohusu kuongeza mkataba baada ya mwezi Januari.
Lengo kuu la klabu ya Arsenal kwa sasa ni kukamilisha uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang, huku dili lao la kumnasa Henrikh Mkhitaryan kwa kubadiishana na Alexis Sanchez likielekea kukamilika.
Swansea italazimika kuvunja rekodi yao ya usajili umrejesha Andre Ayew baada ya klabu ya West Ham kuikataa ofa yao ya pauni milioni 14. (Telegraph)
Chelsea bado ina nafasi kubwa ya kuipata saini ya Peter Crouch licha ya meneja wa Stoke City, Paul Lambert kusisitiza kwamba mshambuliaji huyo raia wa Uingereza hauzwi. (Independent)
Kevin De Bruyne amekubali kusaini mkataba wa miaka sita na klabu ya Manchester City, ambao unaweza ukatangazwa siku ya Jumatatu.
Meneja wa Everton, Sam Allardyce anawania saini ya beki wa klabu ya Lille, Adama Soumaoro.
Ivan Gazidis |
Mkurugenzi Mkuu wa klabu ya Arsenal, Ivan Gazidis yuko Dortmund kukamilisha dili la uhamisho wa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang. (Sun)
Steve McClaren anaema kuwa anataka kurejea kwenye kwenye kazi ya umeneja haraka iwezekanavyo. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 22 Januari, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
1/22/2018 01:42:00 PM
Rating: