Loading...

George Weah kuapishwa leo kuwa rais mpya wa Liberia

George Weah
Raia wa Liberia wanasubiria kwa hamu kuapishwa kwa Rais mpya George Opong Weah.

Wengi wamekesha katika uwanja wa mpira wa taifa, mahala ambapo historia ya mwanasoka huyo inajiandika upya kutoka kung'ara katika soka na hatimaye kuingia katika uga wa siasa kuwa rais wa taifa hilo.

George Weah, maisha yake ya utoto, yalikuwa katika mazingira duni katika mji mkuu wa Liberia Monrovia.

Alipata mafanikio makubwa katika medali ya soka na kufanikiwa kuchezea timu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Chelsea na AC milan.

Ni Mwafrika pekee kuwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa FIFA na tuzo ya Ballon d'Or.

Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa maseneta katika bunge la Liberia.

Aligombea urais mwaka 2005, na alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini akashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki katika duru ya pili.

Aliyewahi kuwa meneja wa George Weah katika klabu ya Monaco, Arserne Wenger amealikwa na atakuwepo katika uapisho huo.

Meneja huyo wa Arsenal alikuwa meneja wa Weah katika klabu ya Monaco inayocheza ligi kuu ya Ufaransa miaka ya 1990 na amesema hakuwahi kufikiria kwamba wakati mmoja mchezaji huyo angekuwa rais.

Huyu ndiye George Opong Weah ambaye leo anaapishwa kuiongoza Liberia.
George Weah kuapishwa leo kuwa rais mpya wa Liberia George Weah kuapishwa leo kuwa rais mpya wa Liberia Reviewed by Zero Degree on 1/22/2018 01:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.