Lissu awasili nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu zaidi
Tundu Lissu amewasili jijini hapo akitokea katika Hospitali ya Nairobi, nchini Kenya alikokuwa anapatiwa matibabu kwa muda wa takribani miezi minne sasa kutokana na kushambuliwa kwa risasi mnamo septemba mwaka jana mkoani Dodoma.
Mbunge Tundu Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka Bungeni, majira ya saa 7 mchana, karibu na nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya madaktari waliokuwa wanamtibu, walieleza kuwa jumla ya risasi 16 zilimpata Tundu Lissu mwilini mwake na wamefanikiwa kuzitoa 15, isipokuwa moja ambayo ipo nyuma ya uti wa mgongo.
Tundu Lissu alieleza kuwa wataalamu na madaktari wake walishauri risasi hiyo ni hatari zaidi kama ikitolewa kuliko ikibaki ndani ya mwili wake kutokana na eneo ilipokwama.
Lissu awasili nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu zaidi
Reviewed by Zero Degree
on
1/07/2018 07:51:00 PM
Rating: