Loading...

Vipimo vyakwamisha uhamisho wa nyota huyu kwenda Real Madrid


Real Madrid imeripotiwa kusimamisha taratibu zote za uhamisho wa golikipa wa Athletic Bilbao, Kepa Arrizabalaga baada ya nyota huyo kugundulika kuwa na majeraha wakati akifanyiwa vipimo.

Kwa mijibu wa taarifa ya tovuti ta 'Sport', Mlinda mlango huyo alifanyiwa vipimo wiki iliyopita na kugundulika kuwa na majeraha yatakayomweka nje ya uwanja hadi mwezi machi.

Inaonekana luwa uhamisho huo unaweza kukamilika kwenye majira ya joto na sio mwezi huu.

Imeripotiwa kwamba, Kepa hayuko tayari kufanyiwa upasuaji akihofia kupoteza nafasi kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uhispania kwenye Kombe la Dunia.

Golikipa wa Athletic Bilbao, Kepa Arrizabalaga
Golikipa huyo anaona ni bora asifanyiwe upasuaji na badala yake akabiliane na tatizo hilo baada ya meneja wa timu yake ya taifa, Julen Lopetegui kuweka wazi kuwa hatapewa nafasi endapo hatacheza mechi nyingi.

Kepa ameichezea klabu yake ya Athletic Bilibao mechi 14 za La Liga kwa msimu huu.
Vipimo vyakwamisha uhamisho wa nyota huyu kwenda Real Madrid Vipimo vyakwamisha uhamisho wa nyota huyu kwenda Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 1/09/2018 08:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.