Loading...

Ajali: Treni ya abiria yaanguka mkoani Kigoma


TRENI ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Tabora kwenda Kigoma imeanguka mchana wa leo kati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amethibitisha.

Hadi sasa hakuna kifo kilichothibitishwa wala idadi ya majeruhi, kamanda huyo ameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye baada ya kufika eneo la tukio.


Kwa mujibu wa shuhuda, ajali hiyo ilitokea mchana wa leo Februari 28, 2018, baada ya mabehewa mawili ya mbele na kichwa chake kuacha njia na kuanguka.
Ajali: Treni ya abiria yaanguka mkoani Kigoma Ajali: Treni ya abiria yaanguka mkoani Kigoma Reviewed by Zero Degree on 2/28/2018 07:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.