Loading...

Mkataba mpya wa Arsenal na Kampuni ya Emirates wavunja rekodi


Klabu ya Arsenal imetangaza mkataba mpya wa udhamini kutoka Kampuni ya Ndege ya Emirates, ambao utadumu hadi kufikia mwaka 2024 na inasemekana una thamani ya zaidi ya pauni milioni 40 kwa kila msimu.

Katika kauli iliyotolewa kwenye tovuti yao, wameuita mkataba huo wa miaka mitano kama “udhamini mkubwa kuwahi kusainiwa na klabu”, ambapo Emirates itaendelea kuonekana kwenye jezi na kwenye nguo za mazoezi za timu hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis ameeleza sababu zilizopelekea klabu hiyo kuamua kuongeza mkataba wa mahusiano na kampuni ya Emirates.


Ivan Gazidis
Kwa mujibu wa taarifa ya NBC, Mkurugenzi huyo alisema: “Mkataba wetu wa udhamini ni mrefu kuliko mingine kwenye Ligi Kuu ya Uingereza na ni moja kati ya mikataba mirefu kwenye ulimwengu wa soka. Mahusiano haya ya pande zote mbili ni ushahidi wa nguvu na kina cha uhusiano wetu wa kipekee. Kwa mara nyingine tena Emirates wameonyesha imani yao kubwa kwetu sisi na ongezeko hilo katika udhamini lilatusaidia kuendelea kushindania mataji na kuleta mafanikio kwa klabu na kwa mashabiki wetu duniani kote.”

Washika bunduki hao pia wamethibitisha kuwa Uwanja wao utaendelea kujulikana kwa jina la 'The Emirates Stadium' hadi angalau mwaka 2028, kutokana na makubaliano yao ya mwaka 2012.

Manchester United ndio inaongoza kwa mkataba wao na kampuni ya Chevrolet, unaokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya pauni milioni 53.01 kwa kila msimu, wakati Chelsea ikiwa nafasi ya pili kwa mkataba wao na kampuni ya Yokohama, unaokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya pauni milioni 40, lakini kwa sasa 'The Gunners' wako sambamba na mahasimu wao wa London.

Manchester City na Tottenham ziko nyuma yao, linapokuja suala la mikataba ya udhamini wa jezi, wakati mkataba wa Liverpool na benki ya Standard Chartered utadumu hadi mwisho wa msimu ujao.
Mkataba mpya wa Arsenal na Kampuni ya Emirates wavunja rekodi Mkataba mpya wa Arsenal na Kampuni ya Emirates wavunja rekodi Reviewed by Zero Degree on 2/20/2018 08:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.