Loading...

Eden Hazard anataka nyota hawa watue Chelsea

Eden Hazard na Nainggolan
Eden Hazard amekiri kuwa angependelea kuona Wabelgiji wenzake, Kevin De Bruyne na Radja Nainggolan wanaungana naye katika klabu ya Chelsea.

Ubelgiji inajiandaa kucheza na Uingereza kwenye Kundi G katika michuano ya Kombe l Dunia 2018 nchini Urusi na meneja wa timu hiyo, Roberto Martinez ana wachezaji wengi kutoka Ligi Kuu ya Uingereza.

Romelu Lukaku ameshafunga magoli 22 katika mechi zote alizoichezea Manchester United msimu huu, wakati Mousa Dembele wa Tottenham anachukuliwa kama kiungo pekee mwenye uwezo mkubwa Ubelgiji.

Kevn De Bruyne
Alipoulizwa ni Mbelgiji yupi angapendelea zaidi kumuona akijiunga na Chelsea, Hazard alimtaja kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne na Nainggolan anayeichezea Roma ya Italia.

“Ubelgiji tunawachezaji, namaanisha wachezaji wazuri. Sio kwamba: “Naichezea Chelsea hivyo sizungumzi na mchezaji kutoka Tottenham” – hapana, tuko pamoja,” Hazard aliiambia COPA90.

“Katima mpira wa miguu, huwa iko hivi kwa sababy, kama haiko hivi, timu zote za taifa zitakuwa kwenye matatizo.”

Nainggolan amekuwa akihisishwa nauhamisho kwenda Stamford Bridge na alikaribia kujiunga na 'The Blues' kuelekea msimu wa 2017/18. Antonio Conte aliweka wazi mapenzi yake kwa Nainggolan na kuthibitisha kwamba, Chelsea ilishindwa kumsajili kiungo huyo.

“Siku zilizopita tulijaribu kumnunua lakini kwa sasa Nainggolan ni mchezaji wa Roma,” Conte aliyasema hayo mwezi Octoba 2017.

“Ninamheshimu sana, naiheshimu sana Roma na wachezaji wake. Sio jambo sahihi kumzungumzia. Hakika ni mchezaji mzuri, kwangu mimi ni mmoja kati ya viungo bora zaidi, lakini ni mpinzani.”
Eden Hazard anataka nyota hawa watue Chelsea Eden Hazard anataka nyota hawa watue Chelsea Reviewed by Zero Degree on 2/28/2018 11:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.