Loading...

Griezmann ana uhakika kwa asilimia mia moja atajiunga na klabu hii kwenye majira ya joto

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Kikatalan, Albert Rogé klabu ya Atletico Madrid imekubali kumuuza Antoine Griezmann kwenye majira ya joto.

Albert anasema kuwa Antoine Griezmann ana uhakika kwa asilimia mia moja za kujiunga na Barcelona kwenye majira ya joto.

Katika ukurasa wake wa mwandishi huyo anadai kwamba, Mfaransa huyo atatua Camp Nou mwishoni mwa msimu huu.

“Dili limemalizika tayari, ingawa ni wazi kwamba hakuna pande yoyote kati ya hizo mbili italizungumzia suala hilo,” aliandika Rogé.

“Tumeshatoa ripoti juu ya kuwepo kwa makubaliano ya siri kati yao wote na kwa asilimia mia moja Griezmann atakuwa mchezaji wa Barcelona kwenye majira ya joto.”

Manchester United ilikaribia kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 – ambaye aliifunga 'hat-trick' wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa goli 5-2 dhidi ya Sevilla Siku ya jumapili – kwanye majira ya joto mwaka 2017, lakini uhamisho huo ulishikwamishwa na adhabu ya Atletico Madrid.

Hata hivyo, hivi karibuni José Mourinho alithibitisha kwamba Mancester United haitapoteza muda kusajili washambuliaji kwenye majira ya joto, na kuipa nafasi Barçelona kufanikisha usajili wa Griezmann.
Griezmann ana uhakika kwa asilimia mia moja atajiunga na klabu hii kwenye majira ya joto Griezmann ana uhakika kwa asilimia mia moja atajiunga na klabu hii kwenye majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 2/26/2018 10:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.