Loading...

Hali ya Kamanda wa Polisi Arusha yaimarika


HALI ya Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo aliyepata ajali eneo la Mdori katikati ya mji wa Magugu na Minjingu mkoani Manyara wakati akisafiri kutoka mkoani Singida kwenda jijini Arusha, inaimarika baada ya kutoka katika chumba cha upasuaji na kupelekwa wodini.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Yusuph Ilembo ameyasema hayo jana jijini Arusha.

Kamanda Mkumbo alipata ajali baada ya gurudumu la nyuma la gari kupasuka na kusababisha lipinduke.

Kiongozi huoy wa Polisi alijeruhiwa kichwani, kidoleni na kufanyiwa ushonaji katika chumba cha uangalizi maalumu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru mkoani Arusha.

Ajali hiyo ilitokea juzi kati ya saa 8 na saa 8.30 mchana.

Alisema kwa sasa, hali ya Kamanda Mkumbo inaendelea vizuri na ameshaondolewa katika chumba hicho na yuko wodi ya kawaida kwa matibabu zaidi katika hospitali hiyo.

Kamanda Ilembo alisema kuwa dereva wa gari la Kamanda Mkumbo aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili PT 2040, Sajenti Silvanus alijeruhiwa mguu wa kushoto na mlinzi wa Kamanda, Magenda hakupata jeraha lolote na wote wako salama.
Hali ya Kamanda wa Polisi Arusha yaimarika Hali ya Kamanda wa Polisi Arusha yaimarika Reviewed by Zero Degree on 2/28/2018 01:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.