Loading...

Huyu ndiye beki wa Leicester City anayempagawisha Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho
Manchester United iko tayari kushindana na klabu ya Manchester City kuwania saini ya beki wa Leicester City, Harry Maguire.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akiwaniwa na vilabu kadhaa kwa muda mrefu, huku klabu ya Leicester ikitaja thamani yake kuwa pauni milioni 50.

Katika harakati za kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ukiachana na Eric Bailly, Chris Smalling na Phil Jones, Jose Mourinho anaweza kugeukia kwa beki huyo, baada ya kusikika hivi karibuni akisema kuwa hatazamii kutumia fedha nyingi tena kusajili mshambuliaji.

Kwa upande mwingine, klabu ya Manchester City nayo bado inatafuta mabeki zaidi, licha ya kusajili beki 
kutoka Athletic Bilbao, Aymeric Laporte, 23  mwezi uliopita.

Harry Maguire
Maguire alijiunga na Leicester City mwaka jana baada ya kuzitumikia Hull City na Wigan Athletic kwa mkopo.
Huyu ndiye beki wa Leicester City anayempagawisha Jose Mourinho Huyu ndiye beki wa Leicester City anayempagawisha Jose Mourinho Reviewed by Zero Degree on 2/12/2018 04:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.