Loading...

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha apata ajali


KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amepata ajali katika eneo la Mdori mkoani Manyara baada ya gari alilokuwa akilitumia kusafiria kupasuka gurudumu ‘tairi’ ya nyuma na kupoteza uelekeo.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Arusha Yusuph Ilembo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Feb 26, 2018 na kusema gari hilo lililokuwa na watu watatu akiwemo msaidizi wakamanda na dereva, lilipata ajali baada ya kupasuka taili ya nyuma na kupoteza mwelekeo.

Mkumbo alipata maumivu kichwani lakini hali zao wote zinaendelea vizuri na wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Mount Meru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha apata ajali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha apata ajali Reviewed by Zero Degree on 2/26/2018 08:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.