Kesi ya Tido Mhando yaahiriswa hadi Februari 28
Tido Mhando akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo |
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Ruswa (Takukuru), Leonard Swai, amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa, kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kumsomea mtuhumiwa huyo maelezo ya awali.
Hata hivyo, Wakili wa Mhando, Ramadhan Maleta, ameieleza mahakama kuwa amechelewa kumuandaa mteja wake kutokana na kuchelewa kupewa maelezo ya awali (Ph) hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa alikubaliana na ombi hilo.
Katika hati ya mashtaka Mhando anakabiliwa na makosa matano yakiwemo matumizi mabaya ya madaraka akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji (TBC).
Kesi ya Tido Mhando yaahiriswa hadi Februari 28
Reviewed by Zero Degree
on
2/23/2018 04:47:00 PM
Rating: