Loading...

Kilichomfanya Wayne Rooney aamue kurejea Everton na si kwenda China


Kiungo mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney, ameeleza sababu ya yeye kurejea Everton na si kwenda China.

Rooney amesema wachezaji wengi wanaocheza katika Ligi Kuu Uingereza hukimbilia katika bara la Asia, pale umri unapowatupa mkono au wanapohitaji fedha.

Kiungo huyo amerejea Everton kutokana na namna ilivyomkuza kabla hajajiunga na Manchester United ambayo imetwaa taji la ligi mara 20.


Rooney amesema kuwa amerudi Everton ili kuwaonesha mashabiki wake kuwa bado anaweza, na atajihidi kuonesha mchango wake ili timu iweze kusonga mbele.

Vilevile ameongezea kwa kusema kuwa ilikuwa maamuzi sahihi kwake kufanya hivyo, anaamini ndani ya miaka miwili, mpaka mitatu ijayo, timu itafika mbali kimafanikio.
Kilichomfanya Wayne Rooney aamue kurejea Everton na si kwenda China Kilichomfanya Wayne Rooney aamue kurejea Everton na si kwenda China Reviewed by Zero Degree on 2/22/2018 11:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.