Loading...

Makamu wa rais wa Marekani agoma kula chakula cha jioni na dada wa rais wa Korea Kaskazini

Dada yake Kim Jong-un akiwa pamoja na Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence
Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence amegoma kuwepo katika chakula cha jioni ambacho alitakiwa kukaa meza moja na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Yong-nam.

Taarifa kutoka chombo cha habari cha Yo hap imesema kuwa Pence alionana kidogo na bwana Kim wakati wakijaribu kukwepana kuonana uso kwa uso.

Wakati huo huo, rais wa Korea ya Kusini, Moon Jae-in ameshikana mikono na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un katika sherehe za ufumbuzi wa mashindano ya michezo ya Olympiki ya msimu wa baridi.

Michezo hiyo inaendelea wakati ambapo kuna mvutano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Pence alimleta Fred Warmbier kama mgeni wa Korea Kusini, baba wa kijana mdogo wa Marekani aliyekufa baada ya kutolewa gerezani huko Korea Kaskazini.

Rais wa Korea ya Kusini Moon Jae-in ameshikana mikono na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini
Bwana Pence na Kim Yong-nam walikuwa wenyeji wa rais wa Korea Kusini kabla ya sherehe haijaanza huko Pyeongchang.

Lakini Makamu rais wa Marekani alikaa kwenye tafrija hiyo kwa dakika tano tu na kuondoka.

Katika shughuli hiyo, Bwana Moon alisema anatarajia mashindano hayo ya michezo ya Olimpiki msimu wa baridi yataweza kukumbukwa kama siku nzuri ya kuanza kuwa na amani.

Hata hivyo ziara hiyo ni ishara kuwa Kim Jong-un yuko tayari kuimarisha uhusiano na Korea Kusini, nchi ambazo zilikuwa katika mvutano kwa kipindi kirefu.
Makamu wa rais wa Marekani agoma kula chakula cha jioni na dada wa rais wa Korea Kaskazini Makamu wa rais wa Marekani agoma kula chakula cha jioni na dada wa rais wa Korea Kaskazini Reviewed by Zero Degree on 2/09/2018 05:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.