Loading...

Mechi yasitishwa baada ya wachezaji 10 kutolewa nje kwa kadi nyekundu nchini Brazil


Wanasoka wa Brazil kwa kawaida wanafahamika kwa ujuzi wao inapokuja katika soka, lakini hakukuwa na cha kuangalia katika mchezo wa soka katika jimbo la Bahia baina ya Vitoria na Bahia.

Baada ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo kilichojaa mshike mshike ambapo wenyeji walipigwa bao na Denilson.

Mambo yalibadilika na kuwa mabaya zaidi baada ya vikosi vya timu hizo mbili kurejea uwanjani kutoka mapumzikoni.

Bahia walipewa penalti katika dakika ya 50 na vurugu zikaanza wakati wageni walipolipuka kwa shangwe na densi mbele ya mashabiki wenyeji.

Wachezaji wa pande mbili wakakusanyika pamoja na kuanza kupigana makonde na baada ya mchezo huo kucheleweshwa kwa dakika 16 maafisa wakijaribu kutuliza hasira - mpiga kipenga akawafukuza uwanjani wachezaji wanane.

Kadi tatu zilitolewa kwa wachezaji wa timu ya Victoria na tano wakapewa wachezaji wa Bahia huku wachezaji wa akiba watatu wakiwemo miongoni mwa waliotolewa nje ya uwanja.

Mechi iliendelea, lakini pale refa alipowapatia wachezaji wawili wa Vitoria kadi dakika 11 baadae waliamua kuondoka uwanjani huku Bahia wakiwa na uwezekano wa kupewa ushindi wa 3-0.


Mechi yasitishwa baada ya wachezaji 10 kutolewa nje kwa kadi nyekundu nchini Brazil Mechi yasitishwa baada ya wachezaji 10 kutolewa nje kwa kadi nyekundu nchini Brazil Reviewed by Zero Degree on 2/19/2018 07:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.