Loading...

Rais Jacob Zuma hali bado tete

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa na jitihada za wapinzani na baadhi ya wafuasi wa ANC, wanaotaka kumwondoa madarakani
Shinikizo linaongezeka dhidi ya rais Jacob Zuma Afrika kusini kujiuzulu, huku maafisa wakuu kutoka chama tawala ANC wakitarajiwa kukutana naye Jumapili kujadili mustakabali wake.

Rais Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa na jitihada za wapinzani na baadhi ya wafuasi wa ANC wanaotaka kumtimua madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, maafisa wa ngazi ya juu wa ANC wana 'jadiliana tu' na rais Zuma kuhusu "ugavi wa uongozi" ndani ya chama.

Lakini nyuma ya kauli hiyo nyepesi - vita vikali vya uongozi vinajitokeza katika nchi hiyo.

Rais Zuma bado yupo madarakani, lakini tangu Desemba mwaka jana, yeye sio mkuu wa ANC tena.

Waendesha mashtaka wakakamavu sasa wanaonekana kushika kasi katika uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa zinazomkabili bwana Zuma na baadhi ya marafaiki zake wa karibu.

Wengi ndani ya ANC wanamtaka rais huyo ajiuzulu haraka iwezekanavyo, ili waweze kujenga upya sifa ya chama hicho kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu nchini mwakani.

Lakini kuna taarifa kwamba rais Zuma anajikita kisawasawa na anatarajiwa kulihotubia bunge wiki ijayo, lakini wafuasi wa upinzani wanataka kumzuia pia, wakieleza kuwa hastahili kusalia kama rais.

Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa, ameshutumu wazi rushwa katika kiwango cha juu ndani ya chama na serikali, lakini anasisitiza kuwa rais Zuma hastahili kuazirishwa.
Rais Jacob Zuma hali bado tete Rais Jacob Zuma hali bado tete Reviewed by Zero Degree on 2/04/2018 06:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.